NEW ALERT

recent
MAHABA

IJUE FAIDA YA NDIMU





NDIMU ILIVYO KIBOKO KWA MARADHI YA JONGO

Maradhi ya jongo (gout) mara nyingi hushambulia vifundo vya miguu, viungio vya magoti, viwiko vya mikono au viungo vingine vya mwili.

Maumivu makali ya viungo husababishwa na chembechembe ndogo za tindikali zinajulikana kama yuriki asidi ndani ya viungo vilivyotajwa, figo na ngozi ya binadamu.

Tindikali hiyo inapokuwa nyingi katika mwili wa binadamu zaidi ya ile inayohitajika, hutengeneza chembechembe kama sindano kwenye sehemu ya viungo tajwa na kusababisha maumivu makali.

Kwa kawaida maradhi ya jongo huwapata zaidi kinababa wenye umri wa kuanzia miaka 35 na kuendelea huku kinamama wale waliokoma kuingia hedhini ndiyo huathirika na maradhi hayo.

Shambulo la jongo mara nyingi huambatana na maumivu makali ndani ya dole gumba la mguuni, joto kali pamoja na uvimbe. Unaweza kupata jongo iwapo utakula kupita kiasi vyakula vya protini na kabohadreti.

Pia kama hutofanya mazoezi vya kutosha, utakunywa vileo kupita kiasi na kuacha kunywa maji ya kutosha. Tumia ndimu iwapo umebaini una tatizo la jongo.

Ndani ya ndimu mna sitiriki asidi yenye uwezo wa kutokomeza yuriki asidi ya ziada ndani ya mzunguko wa damu na hivyo kuifanya ndimu kuwa tiba nzuri ya marandhi ya jongo.Tumia juisi ya ndimu moja ndani ya nusu glasi ya maji asubhi na jioni muda wa siku saba.
Font Awesome Icons
IJUE FAIDA YA NDIMU Reviewed by Admin on 8:00 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.