NEW ALERT

recent
MAHABA

WAJIFUNZE JINSI YA KUMPETI PETI






Kwenye secta ya kumfanya mwanamke apandishe akshi za kimahaba, najua unachojua kukifanya ni kwa kutumia mikono yako. Mdomo wako. Na urimi wako, ila kile ambacho kinamfanya msichana apate hali ya ushawishi na fikra zake kujinyonga kwa huba huku ngozi yake ikisisimka na kupigwa upele wa baridi sidhani kama unakijua. Na nina uhakika kwa asilimia nyingi sana lazima kitakushangaza mno.




Japo mabusu mengi na mitoko ya kimahabaikikamilishwa na maua pamoja na wine ya Dompo au Saint Anna siyo kwamba ni kidogo ukitaka kurudisha huba na husuda, ila kuna njia nyingine rahisi zaidi unazoweza kuzifanya na kukufanya uonekane unavutia zaidi katika secta ya mapenzi na mahaba.




Kiumeni.com kwa upendo wa wasomaji wetu ilibidi kuingia gharama na kualika jopo la wanawake na wasichana toka nyanja mbalimbali ambao wanaumri na mahusiano tofauti tofauti, kama ujuavyo wanawake bila vinywaji vya kuwashitua akili na kuwaweka sawa ili watoe siri zao za ndani sio kidogo, ambapo... usijali tuligharamia, tuliwaweka wazi kuhusu kiini kikuu cha kuwaita sehemu nzuri hio, watueleze ni vitendo gani ambacho wapenzi wao waliwafanyia ambavyo viliwapa cheche za kimahaba na kuwaongezea upendo mara dufu kwa wapenzi wao, ambapo majibu waliyoyatoa hata sie tulikuwa hatukuyadhania pamoja na ukufunzi wetu katika secta ya malavudavyi.




Kila mwanamke alikua na maoni yake na yalikuwa tofauti tofauti, ila tuliyachukua yale yaliyokubaliwa na wanawake wengi zaidi, tulitumia kanuni ya "Wengi Wape!", maoni yalikuwa kama yafuatayo.




1; Usaidizi wa kazi za nyumbani.




Mie nilicheka achana na wewe umetabasamu, ukiwa unamsaidia kazi ambazo huwa unazikwepa na kuona yeye ndo anaetakiwa kuzifanya, inatakiwa uwe unafikilia mara mbili kabla hujapindisha macho yako. "Nikiwa natoka kazini au kwenye pilikapilika na nikamuona akiwa ananisaidia kazi na kunipunguzia mzigo wa kuzifanya, huwa natamani nimrukia hapo hapo alipo, kile kitendo cha yeye kunisaidia kinanipa hisia nzuri, najisikia kama amenitua mzigo kutoka kwenye mabega na pia kitendo hicho hufanya tupate muda wa ziada kufanya yale mambo mengine!" Jesca tokea Dodoma, umri miaka 31 alimaliza kuzungumza huku akiwa na tabasamu jingi. Kwa hiyo jamaa iwapo ukitaka yale mambo yetu uwe unapewa kila utakapo bila kugeuziwa sura "Oooh, mie najisikia vibaya leo nimechoka!", Jamaa inakubidi uyatengenezee mazingira ya kuyapata.




2; Kujitoa.



"Kuna kitu kizuri sana, na huwa inavutia mwanaume anapokuwa muelewa na kujitoa kwenye kile kitu anachokua anakiamini", Naomi miaka 27 kutokea Nyakato Mwanza aliongea. Wanawake husikiliza kwa makini pale unapokuwa unajinadi na unavyomaanisha maneno yako, kitu cha muhimu kwako ni jinsi unavyojitoa kusaidia wengine, inakuwa rahisi pale unapofanya matendo yako yaendane na maneno yako na mwisho wa siku unajikuta umehamsha hisia za mamaa.




3; Ucheshi.




"Mie mwenyewe lazima nikubaliane na hili, kucheka cheka na ucheshi sio karama yangu. Ila huwa kuna kitu flani kuhusu mtu anayeweza kuhadithia kichekesho, akakuvuta mkono na bila kujua anakupiga busu na kukuachia tabasamu, hiyo huwa inanifanya niishiwe nguvu na miguu kupoteza fahamu muda huo huo", alimaliza kutamka Fatuma umri miaka 30. Ukiwa sehemu ya jamii, tafuta jinsi yakumafanya aachie tabasamu, alegeze macho yake na kukuangalia macho ya kungu, tamka kitu kizuri kitakachomfanya achekelee, kitu kinachoweza kumfahamisha japo upo bize na makini na maisha ila ukiwa pembeni yake yeye ndie malikia wako.




4; Uaminifu.




"Nikisikia stori kutoka kwa marafiki na mashoga zangu kuwa anaheshima na ananitunzia heshima japo mie sipo pembeni yake najihisi mwenye bahati maana ninaye mtu wa uhakika", Alisema Joyce kutoka Arusha. Mwanamke anapokuwa na uwezo wa kukuamini iwe yupo pembeni yako au yupo mbali, anakuwa anajiamini pia kukupa mahaba yakutosha maana moyoni anakuwa na amani na wewe, inakuza uhusiano na inasaidia hata mambo yanayotokea juu ya kitanda yawe yafuraha zaidi.




5; Uwezo wa mikono.




Mwanaume anaejua kutumia vifaa vyake nyumbani, anajua pia kuvitumia kitandani. "Boifrendi wangu mie, jamani anauwezo wa kurekebisha kila kitu, sinki, gari, taa!, yaani chochote kile, anatumia hio akili yake ya ufundi kila sehemu mpaka huwa napiga keleleza mahaba jamaniii", Halima wa Makambako alielezea. Hata kama hauna uwezo wa kurudishia redio, ukionyesha umejaribu kufanikisha mambo, mwanamke wako atakuona wewe ni mtu unayeendesha mambo na kusababisha yakamilike.




6; Maneno.




"Nikiwa najitayarisha kutoka au nipo kwenye meza ya vipodozi harafu 
mwanaume akaniambia 'Umependeza' au tu akaninong'oneza masikioni 'Umetoka kimahaba', huwa najihisi siwezi subiri tuwe wawili tuyamalize kitandani, huwa napenda sana !, !", Jacky wa Mbezi umri miaka 25 aliongea. Maneno machache katika wakati muafaka yanaweza kufanya mpenzi wako apagawe na wewe, Nakukumbuka ni kwa kiasi gani alivyokuingia moyoni.



Font Awesome Icons
WAJIFUNZE JINSI YA KUMPETI PETI Reviewed by Admin on 10:02 AM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.