HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUJITIBU MINYOO KWA MAJANI YA MIANZI
HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUJITIBU MINYOO KWA MAJANI YA MIANZI
Minyoo humwingia binadamu anapokunywa maji au anapokula chakula kilichoathiriwa na mayai au mabuu ya minyoo. Pia anaweza kupata minyoo iwapo hatanawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka kujisaidia haja kubwa.
Watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka mitano ambao hupenda kuchezea mchanga au uchafu na wale ambao wanapenda kunyonya vidole wapo katika hatari ya kuambukizwa minyoo kwa urahisi zaidi.
Mambo mengine yanayochangia kushambuliwa na minyoo ni pamoja na kuishi katika mazingira machafu, kutembea pekupeku au kula vyakula visivyoiva au visivyohifadhiwa vizuri huku mlaji akila bila kuvipasha moto.
Zipo aina kadhaa za minyoo ambayo humpata binadamu pia inaweza kuwashambulia wanyama kama ng’ombe, nguruwe, mbuzi, kondoo na hata mbwa.
Kimsingi dalili za minyoo ni pamoja na maumivu ya tumbo, kupata choo kigumu, kupoteza hamu ya kula, kukohoa na kupiga chafya, kuhara, kuwashwa mwili, kujisikia mchovu na mlegevu, tumbo kujaa gesi, kwa watoto kusugua meno, kujipinduapindua wakati mwingine kujikojolea na mwili kudumaa.
Kama ilivyo kwa matatizo mengine ya kiafya yanatibiwa kwa njia mimea asilia, minyoo nayo unaweza kupambana nayo kwa kutumia mianzi na kuimaliza changamoto ya minyoo
Chuma kilo moja ya majani ya mianzi, yaponde na kuyachemsha na lita tatu za maji kwa muda wa dakika 20. Kunywa glasi tatu kwa siku kwa maana ya asubuhi moja, ya pili mchana na ya tatu jioni. Dozi hii ni ya siku tatu.
Ikiwa maji hayo hayajaisha yapashe moto muda wa dakika tano kila unapotaka kunywa. Mara nyingi mianzi ni tiba nzuri zaidi iwapo utabainika kuwa una minyoo aina ya ‘thread worm’.
HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUJITIBU MINYOO KWA MAJANI YA MIANZI
Reviewed by Admin
on
2:38 AM
Rating:
No comments: