NEW ALERT

recent
MAHABA

MAZIWA FRESHI YASIYOTOLEWA MAFUTA YANATIBU MDUDU

MAZIWA FRESHI YASIYOTOLEWA MAFUTA YANATIBU MDUDU

maziwamtindi Instagram posts - Gramho.com

Maumivu makali kwenye ncha ya kidole cha mkononi hususan chini ya ukucha, mara nyingi yanakuwa ni aina fulani ya jipu linalojulikana kama mdudu wa kidoleni.


Tatizo hilo linaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kutumia aina nyingi za tiba ikiwamo asili. Moja ya tiba hizo ni maziwa freshi. Haya yamebainika kuwa ni msaada mkubwa kwa tatizo hilo ambalo humnyima raha mwathiriwa.


Chukua mililita 100 za maziwa yasiyotolewa mafuta, changanya na matone 10 ya mafuta ya nyonyo, kisha lowanisha mchanganyiko huo kwenye kitambaa safi, funga kwenye kidole chenye maumivu.


Kitambaa kinapokaribia kukauka lowanisha mchanganyiko uliobaki na kufunga katika kidole, fanya hivyo wakati wote wa mchana na hata usiku ukiweza. Mara nyingi tiba hii ni ya siku tatu hadi tano utapata nafuu na hata kupona kabisa.


Ikiwa upatikanaji maziwa kwako ni tatizo, tumia unga wa ngano na sukari. Chukua unga wa ngano kidogo changanya na maji kisha korogo hadi uji huo uwe kama tui la nazi.


Baadaye ongeza sukari kidogo na matone 15 ya mafuta ya nyonyo harafu endelea kukoroga kisha uweke jikoni mchanganyiko huo, baada ya kuipua na kupoa hadi hali ya uvuguvugu, chota kiasi uweke juu ya kitambaa kisafi, halafu funga kwenye kidole kinachouma.
MAZIWA FRESHI YASIYOTOLEWA MAFUTA YANATIBU MDUDU Reviewed by Admin on 2:26 AM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.