NEW ALERT

recent
MAHABA

JINSI YA KUTIBU MAJIBU



JUISI YA KITUNGUU MAJI NA SWAUMU INAVYOIVISHA HARAKA MAJIPU

Changanya juisi ya kitunguu maji na swaumu yenye kiasi kinacholingana inayotosha kupaka kwenye jipu siku nzima. Ipake katika jipu mara kwa mara kutwa nzima.


Mchanganyiko huu pamoja na mambo mengine unasaidia kuivisha haraka jipu na kuponyesha baada ya kutumbuka. Baada ya jipu kutumbuka endelea kuosha kidonda na kupaka mchangayiko huo, unasaidia kukiponyesha kidonda kwa haraka zaidi.


Kimsingi jipu husababishwa na vijidudu wanaojulikana kama stafilokokasi wanaoingia kwenye vijifuko vya jasho kupitia kwenye vinyweleo. Jipu ni uvimbe unaoanza sehemu maalumu, mara nyingi linaweza kuwa jipu moja au zaidiu. Uvimbe wa jipu hukua na kisa kutunga usaa na kutumbuka.


Mwanzo jipu huwasha na kisha huwa na maumivu makali hasa linapokuwa sehemu ambayo ngozi yake imebana kama puanini , sikioni, kwapani na katikati ya kidole. Lakini pia jipu linaweza kuota sehemu yoyote.


Mara nyingi chanzo cha jipu ni sumu ndani ya mfumo wa damu inayosababishwa na kutokula vyakula vinavyostahili kwa mwili wa binadamu.


Kama una tatizo lolote la kiafya, karibu kwenye kituo chetu cha kutolea huduma za afya Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam. Acha kuendelea kuteseka kwa maradhi yaliyoshindikana.
JINSI YA KUTIBU MAJIBU Reviewed by Admin on 1:06 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.