HAKI NA WAJIBU WA MUME NA MKE
HAKI NA WAJIBU WA MUME NA MKE
“…Na wanawake wanayo haki(sawa) kama ile haki iliyo juu yao (ya wanaume) kwa wema…” Al Baqarah 228
WAJIBU WA MUME
1 Usimamizi wa familia: Kuhakikisha familia imesimamiwa kikamilifu kwa kufuata misingi ya kiislamu.
2 Huduma: Kuihudumia familia na kuhakikisha mahitaji yote ya kimsingi anayakamilisha kwa njia za halali.
3 Makaazi: Kuhakikisha familia inayo makaazi salama ya kuishi.
4 Kukaa kwa wema: Kuhakikisha anaishi na mke kwa wema na mapenzi na kuhurumiana.
HAKI ZA MUME
1 Utiifu: Ni wajibu wa mke kumtii mume katika mambo yote yaliyoruhusiwa kisheria.
2 Talaka: Ni haki ya mume pekee isipokuwa atatakiwa atumie busara kufikia kuitumia haki hii.
3 Nasaba: Nasaba ya watoto itanasibishwa kwa baba.
4 Hifadhi: Hifadhi ya watoto wakitimia umri wa miaka saba itakuwa kwa baba endapo ndoa imevunjika.

WAJIBU WA MKE
1 Kujisalimisha na kutii: Anapaswa kujisalimisha kwa mume na kuwa mtiifu kwa yaliyoruhusiwa kisheria
2 Kubaki kwenye nyumba: Anapaswa kubakia nyumbani na kutoka kwa idhini ya mume tu.
3 Kujihifadhi na kujisitiri: Anapaswa kutodhihirisha uzuri wa mwili wake kwa asiye maharimu wake.
4 Kuhifadhi nyumba: Kuhakikisha watoto wanalelewa katika maadili ya kiislamu na asitoe kitu chochote ndani mpaka kwa idhini ya mume.

HAKI ZA MKE
1 Mahari: Mahari ni haki yake. Mume au mtu mwengine hana haki yoyote juu ya mahari hii. Kama imetolewa nusu basi ni wajibu wa mume kuhakikisha anaimaliza kwani ni deni kwake.
2 Mahitaji ya lazima: Mume anawajibika kutoa gharama zote za mahitaji ya lazima ya mke.
3 Kuenziwa: Kuenziwa na kujengewa mazingira mazuri ya mapenzi na huba kwa wema
4 Kuonewa wivu: Mke ana haki ya kuonewa wivu usio wa kupindukia.
5 Uadilifu: Ni wajibu wa mume kuhakikisha anafanya uadilifu kati ya wake wenza.
6 Heshima : Mume anawajibika kumuheshimu na kumthamini mke .
7 Khul’u (haki ya kujiachisha): Mke ana haki ya kuomba kujiachisha kwa mujibu wa sheria ikibidi kufanya hivyo.
8 Hifadhi ya watoto: Mke ana haki ya kubaki na watoto mpaka wafike umri wa miaka saba ikivunjika ndoa.

Reviewed by Admin
on
12:39 PM
Rating:
No comments: