MAPOKEZI MAZURI HUINGIZA FURAHA MOYONI
Wakati mume anaporudi nyumbani na kumkuta
mumewe amejiandaa na watoto humkabili kwa
nyuso za bashasha, jambo hilo humuingizia furaha
moyoni mwake. Katika Hadiyth ya Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) tunasoma ya
kuwa,
“Atakayekutana na nduguye Muislamu kwa
alipendalo ili amfurahishe kwa hilo basi Mwenyezi
Mungu Atamfurahisha siku ya Qiyaamah”
Ummu Sulaym, mke wa Abu Twalhah pindi
alipofiwa na mwanawe aliwaambia watu wa
nyumbani kwake,
‘Msimwambie Abu Twalhah hadi mimi mwenyewe
nitakapomweleza’ Abu Twalhah aliporejea kutoka
katika safari zake akamkuta mkewe katika hali
nzuri na sura iliyochangamka.
Abu Twalhah akakaribishwa vizuri na kisha
wakazungumza wakiwa faragha kiasi cha mume
kumaliza haja yake kwa mke wake. Baada ya
hapo ndipo alipomweleza habari ya kifo cha
mwanawe.
MAPOKEZI MAZURI HUINGIZA FURAHA MOYONI
Reviewed by Admin
on
2:35 PM
Rating:
No comments: