MIMBA YA MWEZI WA PILI
Hongera!
Umefikisha miezi miwili ya mimba. Sasa hebu tujadiliane zaidi juu ya maendeleo mwilini mwako na ule wa mwanako katika mwezi huu.
Ukiwa na mimba ya miezi miwili, unaweza kuwa na mchangamko na hisia mbali mbali, wakati mwingine, unaweza kuhisi wasiwasi au kutoamini u mja mzito. Kwa wanawake wengi, Hizi ni hisia za kawaida na ni mabadiliko makubwa katika familia kuweza kupata mwana.
Dalili za mimba ya miezi miwili
Katika mwezi huu wa pili, Una dalili nyingi kama zile za mwezi wa kwanza lakini pia dalili zifwatazo huongezeka kama vile :
- Mhemko wa Hisia
- Ugonjwa wa asubuhi
- Kutamani au kukataa aina ya vyakula
- Uvimbiko
- Kujawa hewa tumboni
- Uchovu
- Kuhisi kizunguzungu
- Uchocheaji wa moyo (heartburn)
- Mikono na miguu kufura
Ingawaje, hisia hizi zote hazileti furaha wala si mazuri kwa mama mzazi, ni za kawaida na hali ya kuwa na mimba. Tuelewe kuwa sio wanawake wote hupitia hisia hizi. Kuna wale waliobahatika na wanaweza kufikisha mimba hadi uzalishaji bila dalili zozote.
Mhemko wa Hisia
Mwezi huu unaweza kuhisi una hisia mbalimbali kama vile unaweza kuwa na hasira ya haraka au bila subira wakati mwingine. Jaribu kupumzika na kuchukulia mambo kirahisi. Kwa sababu ya homoni (human chorionic gonadotropin (hCG), progesterone na estrogen yanazidi kuongezeka mwilini, Usiwe na wasiwasi. Homoni mwilini mwako unaweza kukufanya uwe mtu tofauti na wanawake waliopata mimba hapo awali wanaweza kukusaidia kukumbana na hisia hizi. Ni muhimu mpenziwe kujua kuwa una mimba naye anastahili kuelewa mabadiliko haya ni ya muda chache mwakani.
Ugonjwa wa asubuhi
Ni kawaida kuhisi machungu mwilini wakati wowote wa siku. Kutapika au kuhisi kutapika ni kawaida, kumbuka maumbile ya kila mwanamke ni tofauti.
Ni kawaida mno kubadilisha hamu ya chakula wakati una mimba. Mwezi wa pili huwa na dalili zaidi ya kuwa unapenda vyakula fulani na pia mwili wako hukataa aina fulani vya vyakula. Ni muhimu kujua jinsi ya kula vyakula vilivyo bora ili wewe na mwanawe muwe na afya njema.
Uvimbiko
Katika mwezi huu, unaweza kuendelea kuwa na ugumu wa kuenda chooni. Ni muhimu kunywa maji mengi na kula mboga kwa zaidi. Pia kuna madawa mwanamke anaweza kupewa ili kuimudu mimba yake. madawa haya huwa na vyuma mbali mbali na vinaweza kuzidisha ugumu wa choo. ni vyema kuhakikisha unakunywa maji kila wakati hata usipokuwa na kiu.
Kujawa hewa tumboni
Kwa sababu ya homoni tuliyotaja hapo awali inayojiongeza kila wakati mwilini, Utaweza kugundua umejawa hewa kila wakati na unapitisha hewa kuliko kawaida. Usitie shaka. Haya yote ni ya kawaida. Ni heri kupitisha hewa hii ili usiwe na uchungu tumboni.
“Maria…”Nilipokuwa mja mzito, nilikuwa napitiza hewa kila wakati na ilikuwa vigumu mno kulikomesha. Nakumbuka kuna wakati nilikuwa kanisani na mume wangu, watu walikuwa wamekimya hadi ungeweza kulisikia sindano likianguka sakafuni. Punde tu nilipitiza hewa kwa sauti kubwa. kicheko kilchofuatia kilinipa aibu hadi leo”
Uchovu
Kuelewa ya kuwa mwili wako unapitia mabadiliko mengi sana ili kumhifadhi mwana, Ukisisi umechoka, chukua muda wa kupumzika. Imesemekana kuwa wanawake wenye hupumzika vizuri wakiwa na mimba, huenda kuzaa watoto wenye afya nzuri.
Kuhisi kizunguzungu
Kuongezeka kwa damu na homoni ya pregesterone huwa kizuizi kikubwa cha kupitisha damu kwa haraka, Unaweza kuhisi kizunguzungu wakati nenda wakati rudi, Chukua muda wa kufanya mazoezi kila mchana na pia wakati wa usiku unapolala, weka mto (pillow) chini ya miguu yako ili damu iteremke kichwani. Ukosefu wa damu kichwani ni chanzo kubwa cha kuhisi kizunguzungu. Kula vyakula vyenye huongeza damu mwilini kama vile spinachi, sukuma wiki, maini na kadhalika.
Uchocheaji wa moyo
Kwa sababu ya kuongezeka kwa homoni mbali mbali mwilini, unaweza kuhisi kana kwamba chakula kinarudi juu na kuufanya kifua chako kiwe na uchungu. Hii ni kawaida kwa vile ufuko wa uzazi wako unahitaji nafasi ya mwana kukua kwa hivyo tumbo ya chakula husongea juu kiasi karibu na mabavu na kufanya uwe mwepesi wa pumzi au kuchoka kwa haraka na huenda ukapumua kwa haraka. Ni vizuri kuketi na kupumua hewa kwa undani kabisa na kuutoa polepole. Pia unapohisi kutoa hewa, ni vizuri ili hewa hiyo isijaze tumbo wako na kuleta uchungu mno.
Kufura kwa miguu na mikono
Ni kawaida kwa mwanamke aliye na mimba kufura miguu na mikono kwa sababu ya shinikizo mishipani. Hali hii huenda kuwa zaidi wakati mwanamke anaendeea kuwa mkubwa kimwili. Pia anaweza kuhisi uchungu wa aina mabalimbali wakati mikono na miguu hufura. Kuna wengine ambao huhisi ni kama miguu yao au mikono imelala au vidudu au vipini vyadunga kama sindano. Ndio maanake ni vizuri kufanya mazoezi kila siku na kupumzika kwa wingi.
Kutapika
Ni rahisi sana kwa mama mwenye mimba ya miezi miwili kuhisi kutapika au kutapika kwa uzaidi. Hali hii huendelea hadi mwezi wa tatu au wa nee. Kuna wanawake wengi ambao hutema mate sana sana wakati wamepata mimba. .
Hatua za maendeleo wiki wa tano hadi wa nane?
Kwa wakati huu, mwanao amelazwa vizuri katika mfuko wa uzazi wako. Mfuko huu unamea pole pole ili mwana awe na nafasi nzuri ya kukua. Pia humu ndani ndipo mwana hupata chakula chake na hewa.
Mwanao anatoshana na mbegu ya sesame, pia umbo lake limechukulia ule wa mtoto wa chura. Mwana huyu ameanza kuonyesha umbo la kichwa , mifupa ya mgogo pia umeanza kuumbika na moyo wake pia umeanza kupiga kwa umbali sana.
Mwanzo wa mwezi wa pili mtoto huyu mchanga ana urefu wa milimita moja nukta tano.Karibu na mwisho wa mwezi huu, mwana huyu atakuwa ameongeza urefu hadi milimita kumi na mbili hadi ishirini. Viini vilipotengenezeka hapo mwezi wa kwanza unaanza kubadilika na kuwa viungo.
“Mama hawezi kumkana mtoto, hata akiwa na vilema”
Wiki wa sita
Mtoto huyu ana ukubwa wa mbegu ya ndegu. Mwana huyu ameanza kuutengeneza maumbile kama kichwa, mikono na miguu. Vidole vya mikono na miguu ni kama yale ya bata, Uso ya mwana inaanza kuumbika pia na pua, mdomo na macho yannanza pia kuumbika. Ni vema kujua ya kwamba mtoto huyu ana miezi tisa kukamilika kikamilifu na ni vizuri kujitunza vilivyo. Ukiwa mja mzito, Hali ya kunywa pombe na kufuta sigara huweza kudhulumu ukuaji wa mimba nzuri.
Pia katika mwezi huu ni vigumu kujua kama mimba yako ni msichana au mvulana. Unapoendelea kwa miezi zijazo ambapo tutazungumzia kwa undani, hapo basi utakuja kujua kimakini kuwa una mtoto wa kiume au wa kike.
Mfumo wa (Endocrine) inaaanza kujitengeza, pia sehemu ya moyo umeanza kuumbwa na imegawanyika kwa pande nne. Pia vyombo vya mwili vya mwana vimeanza kutokelezea na ini (liver) imeanza kuwa na chaneli mbalimbali. Ubongo unaanza kuwa mkubwa na unaanza kufanya kazi na pia mikono na miguu ya mwana unaendelea kukuwa. Kwa wakati huu, Mwanako husonga ndani ya mfuko wa uzazi lakini huwezi kumhisi. Anapoendelea kukua, kusonga kwake na kupinduka huwa na nguvu zaidi kwa miezi zijazo na unaweza kumhisi akipiga mateke.
“Mama kwa mwanawe, mtoto kwa mamaye”
Wiki wa saba
Mwanako amefikisha kiwango cha tunda la blueberry na upande wa mkia wake umeanza kupotea kwa upole. mkia huu utapotea pole pole wiko zijazo. ingawaje mikono na miguu yake ni ndogo mno na bado yanaendelea kukua pole pole, ubongo ya mwanao umeanza kufumika pia.
Mfumo wa pumzi pia inaendele kukuzwa, ili pua, mdomo. Koo na chaneli za koo vinaendelea kuumbika usiku na mchana.
Wiki wa nane
Mwanao amefikisha ukubwa wa mbegu ya maharagwe inayoitwa (Kidney bean). kwa wakati huu, kope la macho yamekuwa na karibu mwana yuaweza kufunga majo kikamilifu. pia mkia wake ni mdogo zaidi na karibu upotee kabisa. ubongo wake umeendelea kutengenea chanelli mbalimbali.
Baada ya mwezi wa pili, mwanako ana viungo vya mwili, pia mfuko wa uzazi wako umekomaa na humlisha mwanao kwa kila kitu anachohitaji. Kamba ya umbilical au utovu pia umeanza kuonekana na mwano ameanza kupata chakula moja kwa moja kupitia njia ya chakula unachokila.
Mabadiliko mwilini mwako
Mwezi wa pili wa mimba haina mabadiliko mwilini mwako zaidi ya ule wa mwezi wa kwanza. Lakini, kuna wanawake wengi waliosemekana kuwa na matiti mazito au makumbwa kuliko mwezi wa kwanza. Pia rangi ya chuchu ya matiti yako huwa mweusi zaidi. Unaweza kuonyesha kuwa chuchu yako imekuwa kubwa kiasi na pia pande za mwili kama magoti, tumbo na uso unakuwa na rangi nyeusi kiasi.
Kuna uwezekano wako wa kutoa damu kidogo rangi ya waridi mwezi huu kwa sababu tumbo lako la uzazi linaendelea kupanuka. Usitie shaka kwa sababu kama damu yako si nyekundu kama ya hedhi, ni kawaida. Lakini ukiwa unatokwa na damu nzito na inafananishwa na ule wa hedhi wakati umefikisha mwezi wa pili ya mimba yako, ni muhimu kushauriana na dakitari mara moja.
“Mchea mwana kulia, hulia yeye mkongwe”
Unaweza kuhisi kuenda msaalani zaidi pia kwa sababu ya upanuzi wa tumbo lako la uzazi. Pia damu yako imeongezeka asili mia kumi tangu upate uja uzito.
Katika mfumo wa utumbo, mwanao anakutegemea kwa vyakula bora ili pia naye awe na nguvu ya kuumbika vyema. Ingawaje utumbo wake bado ni changa, mwanako atakutegemea miezi tisa kwa kula na kusiaga vyakula na pia kuenda msaalani. Mwili wako unategemewa na mwana huyu kwa kila kitu hadi atakapozaliwa.
Swala nyeti
Je, ninaweza kula madawa wakati nina mimba?
Kwa muda wa mwezi wa pili, Kuna maswali haswaa ya vyakula ambavyo na vinywaji ambavyo mwanamke anastahili kuvila. kwanza kabisa ni muhimu mwanamke aliye na mimba kukomesha kabisa
- Utumiaji wa sigara
- unywaji wa pombe
- madawa kama vile vya kupunguza maumivu na hata ya malaria
- Kukula vyakula vyenye mafuta mengi
Haya ni kwa sababu ya kumtunza mwana ili asije kuwa na akili pungufu, Magonjwa ya moyo ama ya sukari, kutokua mrefu au sehemu za mwili kutoumbika vizuri. Pia mwanamke anayeendelea na tabia hii huweza kumpoteza mwana kabla ya miezi tisa kufika na ni hatari mwilini mwake.
Upenyo wa haraka
- Unapoendelea katika safari hii, ni vema kujipa neema kwa kila kitu ufanyacho.
- Chukua muda wa kujipa mapumziko,
- Endelea kufurahia na ujue ya kuwa , kuna wanawake wengi wanapitia unachopitia.
- Kumbuka mama yako aliweza kukuzaa na pia kukukuza, pia nawe unapomleta mwana humu duniani, unaweza kuistahimili makumbano yote ya mimba. Endelea kwa ujasiri!
MIMBA YA MWEZI WA PILI
Reviewed by Admin
on
2:42 PM
Rating:
No comments: