NEW ALERT

recent
MAHABA

MIMBA YA MWEZI WA TATU



Hayawi hayawi, huwa!
Amini usiamini, Umefikisha  mimba ya miezi mitatu. Unastahili kuwa mwanamke jasiri kabisa kupitia makumbano ya mwezi wa kwanza na ule wa pili.
 Mfunze mwanao tabia bora kabla kumsahihisha mwana wa mwenzio”
Katika mwezi huu tutajadiliana kwa undani ni mabadiko gani yanaendelea nawe na mwanako, na ni yapi yanaendelea mwilini mwako. Pia tutazungumzia kwa ufupi dalili za mimba ya miezi tatu haswaa kama haukukumbatiana na yale ya dalili za kwanza au ya dalili za mwezi wa pili. Tukumbuke ya kuwa mwili ya wanawake duniani kote wana maumbile tofauti na hupitia njia tofauti wakati wanapokuwa waja wazito.
Hebu tutazame kwa undani:-

Dalili za mimba ya mwezi wa tatu

  • Ugonjwa wa asubuhi
  • kutapika kwa zaidi au kukoma kutapika kabisa
  • Uchovu wa hali ya juu
  • Kuenda haja ndogo kila wakati
  • Uvimbiko
  • Mishipa ya virugu
  • Mishipa ya buibui
  • Kutoa Dutu ukeni (vaginal disharge)
  • Makonda miguuni
  • machungu mgongoni
  • mhemko wa hisia
  • kuongeza kilo
  • uongezaji wa nishati
  • Utulivu
  • Ngozi kubadili rangi

Ugonjwa wa asubuhi

Kabla tuufafanue zaidi dalili hizi, Unaweza kudhani mbona marudio ya yale tuliyozungumzia mwezi wa kwanza wa mimba na ule wa mwezi wa pili.  Utakuja kuona kuwa dalili hizi labda huenda kuongezeka au kupungua kulingana na maumbile ya mwanamke.
Pia kuna dalili zingine huanza kujionyesha wakati mwanamke anapoendelea na miezi yake ya mimba.
Kwa hivyo, mwanamke afikishapo mwezi wa tatu wa mimba, Ugonjwa wa asubuhi huenda kuongezeka au kupungua. Kuna wanawake wengi waliosema wameanza kuhisi nafuu na pia kupata nguvu zaidi. wanawake hawa huweza kurudi kazini.
Lakini kuna baina ya wanawake ambao wakifikisha mwezi wa tatu, wao husikia ni kana kwamba wamekuwa wagonjwa zaidi na wana upungufu wa nguvu. wanawake hawa wanastahili kuchungwa zaidi na pia wanastahili kupata mapumziko zaidi.

Kutapika

Inatufaa tuelewa kama tulivyozungumzia hapo awali kuwa kila mwanamke ana utofauti, Kuna wale ambao wanaweza kuwa na hali ya kutapika zaidi katika mwezi huu.

Uchovu

Ingawaje kuna baina ya wanawake ambao huhisi kuwa wamepata nguvu, Asili mia tisini ya wanawake waja wazito huhisi uchovu mara kwa mara wanapofikisha mwezi wa tatu wa mimba. Hii ni kwa sababu homoni mbali mbali mwilini yanazidi kujiongeza na kumtuza mwana anayekuwa chupani mwa mamake.

Haja ndogo

Chupa cha mwanamke kinapozidi kumkuza mwana, kuenda msaalani kila wakati huwa kawaida. mwanamke aliye mja mzito huweza kuenda haja ndo baada ya muda mfupi tu.

Uvimbiko

Progesterone, homoni inayomsaidia mama kuutunza chupa wake wakati wa uja uzito, pia husaidia kwa kutengeneza maziwa wakati huu, hufanya mwili kuzembea, kwa hivyo, mwanamke huweza kuwa na hewa tumboni na ugumu wa kuenda msaalani. Dalili hii huongezeka kila mwezi na ni muhimu kuzingatia vyakula vipi mwanamke hula. Unywaji wa maji mengi kila wakati ni muhimu zaidi.

Mishipa ya vurugu (varicose veins)

Huenda kuwa baina ya wanawake huanza kuonyesha mishipa hii wanapofikisha mwezi wa tatu wa uja uzito. kwa sababu mwana hulazwa na kuufinya mishipa inayokutanisha roho na miguu, huenda mishipa hii ikifinywa zaidi, damu huteremka pole pole na kuusababisha mishipa kuonekana. Wakati mwingine mishipa hii huweza kumfanya mwanamke kujikunakuna.

Mishipa ya buibui

Mishipa hii huonekana zaidi wakati mwanamke hufikisha mwezi wa tatu wa uja uzito na pia, husababishwa kwa sababu ya kutofanya mazoezi. Kwa hivyo ni muhimu wanawake wanao mimba kufanya mazoezi kila siku na kula matunda vyenye Vitamin C kama vile machungwa, punde tu wanapogundua wameshika mimba.

Kutoa Dutu ukeni

Uke wa mwanamke huendelea kujisafisha wakati anapopata mimba. kwa hivyo ni kawaida kutoa dutu, (vaginal Discarge) iliyo ya kawaida huwa maji maji au kamasi kwa kiasi. Ukiwa na discharge ambayo ni nyekungu, inabidi upate ushauri wa dakitari mara moja!

Makonda Miguuni

Unaweza kuhisi kana kwamba miguu yako yameganda, Pia mikono wakati mwingine. Jaribu kuinua miguu juu wakati unapoketi au unapolala.  Hivyo basi unaweza kuufanya mtiririko wa damu kusafiri mwilini na kuzuia makonda haya.

Machungu mgongoni

Unapoendelea kuwa na mimba, machungu mgongoni husababishwa na kilo cha mwana umbebaye. Uchungu huu huendelea hata baada ya kumzaa mwana. Endelea kufanya mazoezi kila wakati na kujinyoosha kila mara. pia ulalapo, ni vizuri kulala upande wa kushoto wala sio kwa mgongo.

Mhemko wa hisia

Dalili ambayo huendelea hadi unapojifungua ni ule wa hisia zako kubadilika kila wakati.  Furaha, huzuni, mafikira mengi, kulia, kucheka, kuwa mgomvi ni baina za hisia wanawake wengi waja wazito hupitia. Elewa jinsi ya kukumbana na hisia hizi kulingana na uwezo wako mwenyewe.

Kuongeza kilo

Utaanza kugundua ya kwamba umeongeza kilo zaidi kuliko hapo awali. Ni kawaida mwanamke kuongeza kilo kila wiki anapokuwa mja mzito. Huenda kuwa unapohisi unaongeza kilo kwa zaidi ya kawaida ni vyema kumshauri dakitari wako. Pia unapogundua hujaongeza kilo tangu ushike mimba hadi mwezi wa tatu, ni vizuri kupata ushauri wa dakitari mara moja.

Uongezaji wa nishati

Ni kawaida kwa wanawake wengi kuhisi kuwa nguvu zao zinawarudi haswaa mwezi huu wa tatu tangu washike mimba. Ni vizuri kuzingatia kila hali njema ya kufanya kazi haswaa kwa wale wanaofanya kazi ya kubeba vitu vizito au kuinua vitu vizito.

Utulivu

Mwezi wa tatu huja na utulivu wake. Mwanamke ameanza kuzoea maisha ya kuwa na mimba na dalili zake. Kwa hivyo yeye yuajua jinsi ya kujitunza na ni kawaida kuhisi utulivu kwanzia mwezi huu.

Ngozi kubadili rangi

Wanawake wengi wamegundua kuwa wanapokuwa na mimba kuna wakati ngozi yao huenda na kuwa nyeusi. Hii ni kawaida kabisa. Sana sana mwezi wa tatu rangi nyeusi ni kawaida kwa matiti na chuchu chako kuwa kubwa kuliko kawaida.
…Mamu..
Nina watoto watatu, Nilipokuwa mja mzito na watoto hawa, kila mara ngozi yangu ilikuwa nyeusi zaidi. Sana sana tumboni mwangu, matiti yangu, shingoni, magotini. Nilijivisha nguo mrefu ili kuuficha mapacho ya ngozi yangu. Lakini sasa nimetambua kuwa ilikuwa upuuzi tu. kila mwanamke aliye mja mzito ana urembo wake.

Hatua za maendeleo wiki wa tisa hadi kumi na mbili

Wiki wa tisa

Mwana amefikisha kimo cha Inchi moja na ametoshana na tunda la zabibu. Ameanza kufanana zaidi ya binadamu na mwili wake una sehemu zote za binadamu. Moyo ya mwanawe umegawanyika katika mikakati minne.
Sehemu za meno pia zimegawanyika katika kila mwanya ambapo akifikisha umri wa kuonyesha meno, hizo sehemu zitagawanya meno kwa usahihi.
Macho yake yameumbwa kwa ukamilifu, na mkia wake umepotea kabisa. Ana masikio madogo, pua na mdomo.
“Mgoma kutatwa waponzwa na uzazi”

wiki wa kumi

Mwanawe amezidisha kimo cha Ichi moja na ametoshana na matunda ya Lokuats. ( tunda ambalo huliwa bichi na lina rangi ya kibichi wakati ni changa au majano wakati limeiva).
Ameanza kumeza maji. Viuongo vya ndani kama vile figo, matumbo, ubongo na maini (zote zikiwa na seli nyekundu ya damu) yameanza kufanya kazi.
Uti wake wa mgongo sasa umekamilika. Kichwa chake pia kimeumbwa  na ni kubwa zaidi ya pande zote za mwili.

wiki wa kumi na moja

Sasa mwanawe amefikisha kimo cha tini (fig). Ana kimo cha Inchi moja na nusu. Mifupa yake yaliyokuwa mwepesi hapo awali sasa yameanza kuwa ngumu. Yuazunguka tumboni katika kila mfumo nawe huwezi kumhisi hadi wiki zijazo.
Pia kwa sababu diaphram (Upande wa chini wa kifua)  yake imeanza kuumbika, anaweza kuwa na hiccup hapa na pale, Lakini huwezi kumhisi.
Mjukuu kwetu tunda”

Wiki wa kumi na mbili

Mwanao amefikisha kimo cha Inchi mbili na ametoshana na tunda la limao.
kwa wakati huu, mwana yuaweza kufungua na kufunga vidole vyake. Vidole vya miguu pia vyaweza kujinyosha na kujifunga,
Anaweza kulikunja uso wake, na ukilifinya tumbo lako, anaweza kusonga ingawaje huwezi kumhisi. Mdomo wake umeanza kufanya mazoezi ya kunyonya.
Mlimwengu ni mwanawe”

Mabadiliko mwilini mwako

Katika mwezi wa tatu wa mimba, Mwili wako hupitia mabadiliko mengi. Mabadiliko haya huwa ya kawaida. Hebu tutazame baina ya mbadiliko haya.
  • Ingawaje huonyeshi kuwa na mimba haswaa, kiuno cako kimeanza kuwa kubwa.
  • Mhemko wa hisia huongezeka kila mwezi. Na labda umeanza kuonyesha hisia tofauti mwezi huu.
  • Ukienda kumwona dakitari, anaweza kutumia kipimo fulani kusikia upigaji wa moyo wa mwana wako mwezi huu wa tatu
  • Chupa chako kimeongezeka kwa kimo na unaweza kugundua kuwa umeanza kunenepa upande wa tumbo lako.
  • Matiti yako ni makubwa zaidi ya miezi zilizopiata.
  • Kichefuchefu kimeanza kupotea na umeanza kuhisi nguvu. unaweza kufanya kazi bila ugumu na pia unaweza kuanza kula vyakula mbalimbali.
….Tabitha…..
“Nilipofikisha mimba ya miezi mitatu, nilikuwa ninahisi njaa kila wakati. Nakumbuka nikimueleza mama mkwe kuwa nahitaji kula ugali na nyama wakati wa asubuhi na kuongezea, maziwa mala. Mume wangu alishangazwa na tabia hii lakini aliniunga mkono kwa sababu nilikuwa nambeba mtoto wetu”

Swala nyeti

Je ni siku ipi nzuri ya kueleza familia na marafiki kuwa nina mimba?
Kwa wanawake wengi, Swala hili limechukuliwa kwa wazi. Kuna wale ambao hutangaza punde tu wanapokosa hedhi na kuna wale wanaongoja hadi mwezi wa tisa kueleza kuwa wanamtarajia mwana.
Ni vizuri kungoja hadi mwezi wa tatu ili kutangaza una mimba kwa sababu hali ya mwili wako sasa umeanza kurudi kuwa ya kawaida na hofu ya kumpoteza mwana umeanza kudidimia.
 Mtoto anampenda mama”

Upenyo wa haraka

  • Mapumziko ni ya lazima mwezi huu.
  • kufanya mazoezi na kunywa maji mengi ni muhimu sana.
  • Kula matunda mengi yenye Kalsiamu, vyakula vyenye vyuma ili kuongeza damu.
  • Jaribu kujinyoosha kila mara.
  • Tembea kwa muda wa nusu saa kila siku.
Sura ifwatayo tutaendelea kunena juu ya mabadiko yapi yanaendelea na mwanako na mwilini mwako.
Kwa wanaume wanaotarajia wana, Ni muhimu kujua yale yote mwanamke hupitia akiwa na mimba ili kuwe na maelewano baina ya wapenzi hawa.
Kumtunza mwenziwe wakati anapotarajia mwana ni muhimu ili kupunguza mafikira kwa mwanamke ili mwana aweze kukua vizuri.
Ungana nasi tutakapojadiliana mimba ya miezi minne.
MIMBA YA MWEZI WA TATU Reviewed by Admin on 12:34 AM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.