BAADHI YA MAMBO YANAYOSTAWISHA MAHUSIANO NA NDOA
1. Kamwe msiweke siri kati yenu, kuwa mahali ambapo umemwambia utakuwepo, msidanganyane.
2. Siku zote mkumbatiane na kum kiss kabla hamjaondoka nyumbani kwenda kwenye mihangaiko.
3. Mwenzako anapoongea, usitumie masikio tu kumsikiliza. Tumia na moyo wako pia.
4. Kamwe msiongelee mambo yaliyopita katika mahusiano yenu, mjikite katika future yenu. Ya kale hayana faida.
5. Siku zote mle pamoja kama kuna uwezekano huo na mlale pamoja kila usiku!
6. Tenga muda wako wa weekend kwa ajili ya familia yako, kuwa karibu na mpenzi wako na wanao kama unao!
7. Kama mko mambo safi sio mbaya mkaenda hata nje ya mji mnaoishi, wawili tu mkafurahia weekend yenu huko sehemu tulivu. Hii inaamsha mapenzi upya.
8. Kama unataka mabishano fanya hivyo kwa busara na kwa hoja, usifanye papara jifunze kunyamaza na kusikiliza.
9. Siku zote jikumbushe kwamba mapenzi ya kweli ni adimu kuyapata, hauwezi kupata mwingine atakaekupenda kama huyo, jifunze kumpenda, ukishindwa nae atajifunza kukuacha uende!
10. Siku zote simamia maneno yako na ahadi zako. Usiyumbishwe na jambo lolote lile.
Nimezungumza vyema?
Nimezungumza vyema?
BAADHI YA MAMBO YANAYOSTAWISHA MAHUSIANO NA NDOA
Reviewed by Admin
on
10:46 AM
Rating:
No comments: