UNAJUA JINSI YA KUTIBU MAGONJWA YASIO ONEKANA
MAJANI YA BAHARI YANAVYOSAIDIA MAGONJWA YASIYOONEKANA KATIKA VIPIMO VYA KISASA
Kuna magonjwa ya aina mbalimbali yanayowasumbua wanajamii kila kukicha. Watalaamu wa huduma za kisasa na wale wa asili usiku na mchana wanahangaika kuwaponyesha.
Miongoni mwa magonjwa hayo yapo ambayo mtu anaumwa lakini akienda kupata vipimo vya kisasa ili kuyabaini, hayaonekani katika vipimo huku akiendelea kuhangaika kwa maumivu.
Leo nazungumzia namna ya kukabiliana nayo ambapo yanasababishwa na sababu nyingi ikiwamo kutofanya mazoezi ya kutokwa jasho.
Zipo namna nyingi za kuondokana na magonjwa hayo, binafsi nitazungumzia njia mbili ambapo ya kwanza ni ya Sauna, huu ni mfumo ulioandaliwa kitaalamu ambao unamfnya mtu atokwe jasho.
Njia ya pili ni kutumia majani yaliyoota ukingoni mwa baharia au yale yaliyombwa na maji bahari kutoka mbali.
Baada ya kupata majani hayo yaweke katika chombo iwe chungu au sufuria, tia lita tatu hadi tano za maji kisha bandika jikoni. Hakikisha yanachemka vya kutosha kisha yaipue ukiwa bado umeyafunika.
Chukua shuka zito au blanketi jifunike sehemu yalipo majani hayo kisha funua chombo ulichoyafunika huku ukihakikisha mvuke wake unakupata vizuri mwilini. Fanya hivyo kila siku asubuhi na jioni muda wa siku saba. Utafurahia nafuu hata uponyaji wa maradhi hayo.
UNAJUA JINSI YA KUTIBU MAGONJWA YASIO ONEKANA
Reviewed by Admin
on
1:54 AM
Rating:
No comments: