NEW ALERT

recent
MAHABA

JINSI YA KUPEVUSHA MAYAI KWA KINAMAMA

NYANYA MAJI INASAIDIA KUPEVUSHA MAYAI KWA KINAMAMA

Kupevuka kwa yai - Ovulation - Afya Track
Nyanya maji ni tunda lenye rangi nyekundu, lina maumbo tofauti kulingana na aina ya mbegu iliyopandwa eneo husika. Zipo nyanya zenye umbo mviringo, nyingine ndefu, zipo pia zile ndogo za asili zinazofanana na goroli.

Nyanya ambayo ni kiungo maridhawa cha vyakula, imekuwa ikijizolea umaarufu maeneo mengi nchini na kwingineko duniani kila kukicha. Pamoja na kuwa ni kiungo cha vyakula, pia ni nzuri kwa kutengenezea kachumbari na saladi.

Hata hivyo, wakati nyanya maji ikijijengea umarufu kwa kuwa ni kiungo, kwa upande mwingine ni tiba ya maradhi mbalimbali yanayomsumbua mwanadamu wa leo.


Nyanya maji inasaidia kupevusha mayai kwa kinamama, kupambana na shinikizo la damu, kumeng’enya chakula, juisi yake ni chanzo cha ngozi yenye mvuto na laini. Nyanya maji inajulikana kwa kuwa na wingi wa vitamini A, B1, B2, B3, B6, C na K pamoja na madini ya chuma, shaba, phosphorus, Potassium, manganese na protini.


Pia nyanya maji inasaidia kuboresha kinga za mwili na kuongeza uwezo wa uoni, inaondoa sumu mwilini na ina ‘lycopene’ ambayo ina uwezo mkubwa wa kutengeneza seli nyekundu za damu na pia kuondoa mafuta kwenye mishipa ya damu.


Tumia juisi yake kutwa mara tatu au nyanya ya unga uichanganye na asali kisha tumia kutwa mara tatu.


Nyanya maji unaweza kuitumia ile iliyosagwa kwa kuichanganya na chakula unachotaka kula, pia inasaidia kuondoa na kukinga matatizo mengi ya kiafya. Ifanye nyanya maji kuwa chakula na kinywaji chako cha daima utafaidika nayo kwa mengi.


Aidha kwa mtumiaji ni vema aioshe nyanya maji kabla ya kuitumia kwa kuitengenezea juisi, au kupata unga wake au kuungia kwenye chakula kwa kuwa baadhi zinawekewa dawa za kuulia wadudu zinapokuwa shambani ambayo inaweza kuwa na athari kwa afya ya mlaji.
JINSI YA KUPEVUSHA MAYAI KWA KINAMAMA Reviewed by Admin on 6:12 AM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.