NEW ALERT

recent
MAHABA

TATUA TATIZO LA BAWASIRI


Bawasiri (kikundu) ni hali ya kutoka kinyama mfano wa utumbo sehemu ya haja kubwa. Tatizo hilo linalowapata watu wa jinsia na rika zote, mara nyingi limekuwa kikwazo kwa wagonjwa wanaokabiliwa nalo.

Kikwazo kinakuja kutokana na kuwepo dhana miongoni mwa watu kuwa tatizo la bawasiri lina uhusiano na kufanya mapenzi kinyume na maumbile miongoni mwa wagonjwa dhana ambayo haina ukweli wowote.

Kutokana na dhana hiyo, baadhi ya waathiriwa huogopa kujitokeza kupata tiba kwa kuogopa kuchekwa hivyo kubaki wakiteseka na tatizo hilo kwa muda mrefu.

Kimsingi ugonjwa huu unatokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ndani na nje ya haja kubwa. Wakati mwingine mishipa inaweza kupasuka na kusababisha kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa.

Chanzo cha bawasiri wakati mwingine kinaweza kuwa ni matatizo ya kufunga choo, kusimama au kukaa kwa muda mrefu, kazi za kutumia nguvu kubwa, udhaifu wa misuri ya mwili au unene kupita kiasi.

Ugonjwa huu unaweza kutibiwa kwa ganda la komamanga. Kaanga ganda la komamanga bila mafuta hadi liwe jeusi, baadaye saga ili kupata jivu laini. Changanya na mafuta ya karanga au pamba kisha ingiza katika njia ya haja kubwa mara mbili kutwa.

Zingatia maelekezo ya mtaaalamu unapotumia dozi hii. Tumia mfululizo kwa muda wa siku 10 utakuwa umepata nafuu au kupona kabisa, ikiwa tatizo linaendelea unaweza kuongeza siku 10 nyingine.

Au unaweza kutumia maji ya mgomba kukabiliana na tatizo hilo. Chukua maji ya mgomba paka sehemu ya haja kubwa kutwa mara tatu kwa maana ya asubuhi, mchana na jioni. Dozi hii ni ya siku saba mfululizo.
Font Awesome Icons
TATUA TATIZO LA BAWASIRI Reviewed by Admin on 7:16 AM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.