NEW ALERT

recent
MAHABA

WANAWAKE WENYE KUJIHIFADHI HUPATA RADHI ZA ALLAAH



WANAWAKE WENYE KUJIHIFADHI HUPATA RADHI ZA ALLAAH

Allaah anasema
{Ee Mtume waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu wajiteremshe uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapeleka upesi wajulikane (kuwa ni watu wa heshima) wasiudhiwe. Na Allaah ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu} [Al-Ahzaab 33: 59].

Hijaab ni lazima! Allaah سبحانه وتعالى Anasema:

{Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Allaah, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa} [An-Nuwr 24: 31].

Hiyo ni kinyume na vile wanawake wakisasa walivyo. Wao hutoa visingizio kwa kutovaa Hijaab inayotakikana. Mtume صلى الله عليه وسلم alisema:

“Kikundi cha wanawake hawatoingia peponi. Hao ni miongoni mwa wale wanaovaa nguo za kubana, za kuonyesha mwili na hawafuati amri ya Allaah سبحانه وتعالى ya kuvaa Hijaab. Hawataingia tu peponi bali hata hawatasikia harufu ya pepo ambayo harufu yake husikilizana masafa ya mwendo wa miaka 500.” [Muslim].

Mwanamke ambae anadai kuwa kitu muhimu ni nia yake, na kuwa dhamira yake sio mbaya na kuwa yeye ni mtu mzuri, na kuwa Hijaab ni ya moyo. Mwanamke huyo huyo anadai kuwa anaswali swala tano, sunna na swala za usiku na anatoa sadaka. Kweli anafanya yote hayo, lakini kisha anasema ibada hizo zinatosha. Subhana Allaah! Kasema Allaah سبحانه وتعالى:

{Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakataa baadhi yake? Basi hana malipo mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila hizaya katika maisha ya duniani, na Siku ya Qiyaamah watapelekwa kwenye adhabu kali kabisa. Na Allaah si mwenye kughafilika na yale mnayo yatenda}. [Al-Baqarah 2: 85].

Mtume صلى الله عليه وسلم amesema:

“Moto umezungukwa na matamanio yetu, na pepo imezungukwa na juhudi zetu.”

Bado unaona tabu kuvaa Hijaab, unaona tabu kufuata maamrisho ya Allaah سبحانه وتعالى .

Nani atatahayuri wakati huo? Yule ambae anaonesha mapambo yake kwa kila mtu au yule anaejistiri na kujiheshimu?

Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: “Ukamateni Uislamu na mikono yenu na meno yenu”.

ALLAAH ATUPE IMANI NA ATUONGOZE KATIKA KUFUATA QURAN NA SUNNA



Font Awesome Icons
WANAWAKE WENYE KUJIHIFADHI HUPATA RADHI ZA ALLAAH Reviewed by Admin on 10:24 AM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.