FAIDA YA MAJI MOTO
MAJI YA UVUGUVUGU MSAADA KWA NYAYO ZINAZOWAKA MOTO
Matatizo ya miguu hadi nyayo kuwaka moto mara nyingi huwapata watu ambao shughuli zao zinawalazimu kutembea au kusimama kwa muda mrefu huku miguu ikiwa imening’inia.Miguu na nyayo kuwaka moto kunasababishwa na mzunguko dhaifu wa damu kwenye miguu na ukosefu wa virutubisho na madini yanayohitajika kwenye mwili kwa kuwa chakula kinachotumiwa hakifai kwa afya bora.
Chakula cha asili kinahitajika zaidi kuondoa sumu zinazoleta athari kwenye mwili pamoja na kufanya mabadiliko katika aina ya vyakula vitakavyoliwa kwa ajili ya kupata virutubisho na madini muhimu.
Ukibaini una tatizo hilo tumia maji ya uvuguvugu na chumvi kuondokana nalo. Ukiwa umekaa, tumbukiza miguu ndani ya maji ya uvuguvugu yaliyoongezwa chumvi ya mawe yakiwa ndani ya karai muda wa nusu saa.
Ukiwa umetumbukiza miguu kwenye karai hilo osha kwa maji hayo sehemu zote zinazouma au kuwaka moto ambayo maji hayo hayakuzifikia, endelea hadi magotini.
Fanya hivyo mara tatu kutwa. Kwa kawaida tiba hii imeleta matokeo mazuri kwa waliotumia kwa kuzingatia maelekezo ya mtaalamu.
FAIDA YA MAJI MOTO
Reviewed by Admin
on
3:03 PM
Rating:
No comments: