NEW ALERT

recent
MAHABA

MUWASHO SEHEMU YA HAJA KUBWA



TUMIA GANDA LA KOMAMANGA KUONDOA MWASHO SEHEMU YA HAJA KUBWA



Sehemu ya kutokea haja kubwa inaweza kuwa na mwasho wa mara kwa mara kama ilivyo kwa sehemu nyingine za mwili wa mwanadamu. Kuwashwa sehemu yoyote ya mwili inaweza kuwa ni matokeo ya tatizo lililoko mwilini kama vile minyoo au mzio.


Nikiwa mtaalamu wa tiba lishe na virutubisho asilia, nashauri unapoona una mwasho wa aina yoyote katika mwili wako, ni vema nenda kafanyiwe uchunguzi na mtaalamu kabla ya kuanza tiba.


Aidha, kwa tatizo la kuwashwa sehemu ya kutolea haja kubwa, unaweza kutumia ganda la tunda la komamanga. Oka ganda la komamanga hadi liwe jeusi, saga kupata jivu laini.


Changanya kidogo jivu hilo na mafuta ya karanga au ufuta kisha paka sehemu yote ya haja kubwa inayowasha. Fanya hivyo asubuhi na jioni mfululizo muda wa siku saba. Kimsingi kuwashwa sehemu ya kutokea haja kubwa ni dalili ya kuwa na minyoo sindano.


Kama una tatizo lolote la kiafya, karibu kwenye kituo chetu cha kutolea huduma za afya Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam. Acha kuendelea kuteseka kwa maradhi yaliyoshindikana.


Tunamjali mgonjwa yeyote, tunatumia tiba lishe na virutubisho asili kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya zinazomsumbua binadamu.
MUWASHO SEHEMU YA HAJA KUBWA Reviewed by Admin on 12:55 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.