NEW ALERT

recent
MAHABA

IJUE FAIDA YA PAPAI KWENYE NGOZI YAKO





PAPAI HUEPUSHA MAGONJWA YA MARA KWA MARA

PAPAI ni tunda lisilo geni miongoni mwa Watanzania wengi. Ardhi yenye rutuba inaifanya Tanzania kustawisha aina nyingi za matunda likiwamo papai.


Asili ya papai ni Kusini mwa Mexico na Amerika ya Kati. Hata hivyo, kwa sasa tunda hilo linalopatikana sehemu mbalimbali duniani. Baadhi ya watu wamekuwa wakilitumia papai kutatua tatizo la kukosa au kulainisha choo.


Hii ni kwa sababu ya kuwa na nyuzinyuzi lishe ‘fiber’ ambazo zinasaidia katika umeng’enyaji wa chakula tumboni. Kwa upande mwingine papai linapotumiwa kwa kuzingatia maelekezo ya watalamu linasaidia watu wenye uzito mkubwa kuondokana na tatizo hilo.


Uwezo huo unatokana na tunda hilo kuwa na kirutubisho kinachoitwa ‘calories’ na ‘fiber’. Mbali na faida hizo, papai pia linasaidai kuimarisha kinga za mwili na kumfanya mtumiaji kutozongwa na magonjwa ya mara kwa mara.

Papai moja lina asilimia 200 ya mahitaji ya kila siku ya vitamini C, hivyo kuufanya mwili kujenga uimara wa kinga zaidi. Kwa watu wenye matatizo ya kisukari wanashauriwa kutumia papai kwa kuwa ni miongoni mwa matunda yenye kiwango cha chini cha sukari, licha ya kuwa na ladha tamu.


Mgonjwa wa kisukari anaweza kula japo kipande kimoja cha papai kila siku ili kunufaika na tunda hilo. Ulaji wa papai pia unasaidia kuimarisha afya ya macho (uoni), hii ni kutokana na kuwa na vitamini A ya kutosha. Aidha, papai ni moja ya matunda yanayosaidia kuboresha afya ya ngozi kwani linaondoa mikunjo katika ngozi.


Hii itakubidi utumie kwa muda wa wiki mbili mfululizo. Ni tiba lishe iliyosheheni virutubisho na madini ambayo yanasaidia kuondoa maumivu ya mwili na kurekebisha kiwango cha insulin mwilini, hivyo ni kirutubisho rafiki kwa wagonjwa wa kisukari pia.


Matumizi yake husaidia kuongeza hamu ya kula pamoja na kupunguza kiwango cha lehemu (cholesterol), mwilini huku kikimwacha mtumiaji akiwa mchangamfu.

Ili tunda hilo likusaidie kutunza ngozi yako; kipande kimoja cha papai changanya na unga wa ngano kijiko kimoja halafu paka mchanganyiko huo sehemu iliyoathiriwa (yenye mikunjo) kisha uache mwilini muda wa dakika zisizopungua 10 halafu nawa kwa maji safi na salama.


Fanya hivyo japo mara moja kwa siku ikiwezekana iwe usiku kabla ya kulala, na baada ya siku kadhaa utaanza kuona mabadiliko katika ngozi yako. Mbegu za papai zikisagwa baada ya kukaushwa kivulini weka kijiko kidogo cha unga wake kwenye kikombe cha uji uzio mzito unasaidia kuondoa tatizo la minyoo.
Font Awesome Icons
IJUE FAIDA YA PAPAI KWENYE NGOZI YAKO Reviewed by Admin on 1:44 AM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.