MALIZA MAUMIVU YA HEDHI KWA NIA HII
KOMAMANGA TUNDA LINALO TULIZA MAUMIVU YA HEDHI
Komamanga ni tunda linalopatikana katika baadhi ya maeneo nchini, asili yake ni Iran na Kaskazini mwa India. Mkomamanga unasifika kwa kuhimili hali ya hewa ya ukame.
Miongoni mwa virutubisho vinavyopatika katika komamanga ni pamoja na vitamini A, B5,C, E pamoja na madini ya potassium na ya chuma. Katika tiba, komamanga linatumika kama huduma ya kwanza kukabiliana na tatizo la kutokwa na damu ya hedhi kwa muda mrefu.
Unachopaswa kufanya ni kuandaa juisi yake, mpe mgonjwa glasi moja asubuhi wakati wa kifungua kinywa kila siku muda wa wiki moja mfululizo.
Kwa mwenye tatizo ni vema aanze mchakato huo siku tatu kabla ya kuanza hedhi, ikiwa tayari analijua tatizo lake na endapo lilishatokea siku za nyuma, aendelee na tiba hiyo hadi siku mbili mbele baada ya damu kuacha kutoka.
Wanashauriwa kutumia juisi yake japo glasi mbili kila siku asubuhi na jioni muda wa wiki mbili. Komamanga pia linasaidia kulinda afya ya kinywa na meno kwa kuzuia kuoza na kuhuisha mfumo wa kinga za mwili kwa kuondoa vijidudu na maambukizi ya virusi ndani ya mwili.
Halikadhalika linasaidia kurekebisha maradhi ya tumbo kama kuharisha na kutopata choo endapo juisi yake itatumiwa kwa kuzingatia maelekezo ya mtaalamu.
Majani ya komamanga nayo yanasaidia kutoa ahueni kwa mgonjwa wa malaria au homa. Yaoshe vizuri, yachemshe, mpe mgonjwa anywe glasi ya maji hayo moja asubuhi na nyingine jioni muda wa wiki mbili mfululizo.
Tunda hili pia lina uwezo wa kuzuia shinikizo la damu mwilini pamoja na mrundikano wa sumu. Ni kirutubisho kilichoandaliwa kwa mimea tiba ambacho husaidia matatizo mbalimbali ya kinamama kama vile chango la aina yoyote na kuondoa sumu mwilini.
Kunywa glasi moja ya juisi ya komamanga kila siku inasaidia kumpunguzia mtumiaji hatari ya kukumbwa na tatizo hilo. Pamoja na hayo, tumia mara kwa mara tunda hilo hasa juisi yake linasaidia kuimarisha mfumo wa kinga ndani ya mwili na kumfanya mtumiaji kutozongwa na magonjwa ya mara kwa mara.
Komamanga pia linasaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa jinsia zote hii ni kutokana na kuwa na kirutubisho ‘antioxidants’ ambacho kinasaidia kuboresha mzunguko wa damu mwilini.
MALIZA MAUMIVU YA HEDHI KWA NIA HII
Reviewed by Admin
on
6:51 AM
Rating:
No comments: