JINSI YA KUZUIA KIFAFA CHA MIMBA
HII NDIYO NYANYA PORI INAYOZUIA KIFAFA CHA MIMBA
Nyanya asili (nyanya pori) ni moja ya mazao ya bustani ambalo baadhi ya wakulima hawalipi kipaumbele. Sijui ni kwanini labda ni kutokujua faida zake.
Aina hii ya nyanya ina manufaa makubwa kwa afya ya binadamu. Ikitumiwa na mama mjamzito katika chakula bila kuongeza kiungo kingine iwe nazi au mafuta inamsaidia kuepukana na shinikizo la damu na kifafa cha mimba kwa kuwa ina utajiri wa kirutubisho kinachojulikana kama lycopern ambacho kina uwezo wa kuondoa mafuta kwenye mishipa ya damu.
Kimsingi ukitaka kuungia nyanya hizi katika chakula usitoe mbegu wala kumenya maganda badala yake viliwe vyote kwa kuwa vina manufaa makubwa katika mwili wa binadamu.
Majani ya nyanya hizi zenye umbo dogo ambapo wakati mwingine unaweza kuzifananisha na golori, ukipika pamoja na mboga nyingine yanasaidia kuondoa maumivu ya tumbo.
Mara nyingi nimekuwa nikisisitiza jamii itumie chakula kama dawa ili kuukinga mwili na magonjwa badala ya kutumia dawa kama chakula.
Kwa kawaida aina hii ya nyanya ni zile ndogondogo ambapo miaka ya nyuma kabla ya kuenea kwa kilimo cha nyanya za kisasa, zilikuwa zikiota porini au wakati mwingine zilioteshwa maeneo ya wazi kwenye makazi ya watu.
Ni kiungo kizuri kwa vyakula vya aina mbalimbali, watoto wadogo pia hupenda kula kwa sababu zikiwiva zinaonekana kama matunda na ukila hazina radha tamu kama sukari pia hazina ugwadu.
Kiungo hiki muhimu miaka ya hivi karibuni kimeonekana kudharauliwa na watu wengi hasa baada ya nyanya kubwa kupata nafasi katika jamii.
Wapo baadhi ya watu wamekuwa wakiziona kama zimepitwa na wakati bila kujua kuwa ni msaada mkubwa katika miili yao.
Juisi ya majani yake ni dawa kwa wenye matatizo ya kikwapa wapake jioni hadi tatizo hilo litakapokwisha, pia yanaponyesha haraka kidonda kibichi iwapo utapaka juisi hiyo.
Mizizi ya nyanya hizi baada ya kuichemsha maji yake yanasaidia kuondoa vimbe ndani ya tumbo la uzazi. Nyanya hizi pia zina vitamini A, B6, C na E, zinaondoa sumu mwilini rangi nyekundu katika nyanya hizi ni dawa ambayo inaondoa mafuta na sumu mwilini.
Namna ya kutengeneza chukua nyanya nane ondoa vikonyo changanya na unga wa pilipili manga robo kijiko cha chai na maji robo lita kunywa juisi hiyo kutwa mara tatu asubuhi, mchana na jioni, muda wa siku 14.
JINSI YA KUZUIA KIFAFA CHA MIMBA
Reviewed by Admin
on
1:59 AM
Rating:
No comments: