Ondoa maumivu ya viungo kwa kula chenza
Ondoa maumivu ya viungo kwa kula chenza
Chenza ni tunda jamii ya chungwa. Licha ya maeneo mengi yanayostawishwa machungwa, machenza nayo hupatikana, lakini si kwa wingi kama ilivyo kwa machungwa.
Kama mara nyingi ninavyozungumza tutumie chakula kama dawa badala ya dawa kama chakula. Tunda hili tamu lina faida nyingi kwenye mwili wa binadamu ikiwamo vitamini C, linazua damu kuvuja katika fizi, lina imarisha mifupa, linaongeza nguvu katika misuri na kuondoa maumivu ya viungo.
Chenza linaondoa baridi yabisi, viuvimbe chini ya tumbo, mawe katika figo, kusafisha kibofu cha mkojo, linasaidia kupunguza unene na kuondoa uoni hafifu katika macho. Ili kunufaika na faida tajwa ni vema ukala tunda lenyewe lililowiva na si vinginevyo.
Nimesema hivyo kwa sababu baadhi ya watu ukiwauliza unapokula tunda fulani unanufaika na nini atakuambia nalipendea utamu wake. Anayekula tunda kwa sababu ya utamu pekee hawezi kulitilia maanani ya kulila ipasavyo ili kunufaika na faida zake, hivyo ni vema ajue utamu na faida anayoweza kuipata kwa kula tunda husika.
Ondoa maumivu ya viungo kwa kula chenza
Reviewed by Admin
on
2:30 AM
Rating:
No comments: