NEW ALERT

recent
MAHABA

KAMA UNA JIPU FANYA HIVI



TUMIA JANI LA TAMBUU AU WENGINE WANAPENDA KUUITA MPOPO KUIVISHA JIPU HARAKA


Jipu husababishwa na vijidudu wanaojulikana kama ‘staphyylococcus’ ambao wanaingia kwenye ngozi kupitia vijimfuko vya jasho kupitia kwenye vinyweleo. Kwa kawaida uvimbe wa jipu huanza sehemu moja.

Jipu linaweza kuwa moja au zaidi. Uvumbe wa jipu huendelea kukua na kisha kutunga usaa ambao baadaye hutumbuka. Jipu linapoanza linaweza kuonesha hali ya kuwashawasha baadaye huwa na maumivu makali hasa linapotunga sehemu ya mwili iliyobana kama kwapani, puani au sikioni.

Kimsingi majipu hupendelea kutokeza sehemu za usoni, shingoni, makalioni, mapajani au sehemu nyingine yoyote katika mwili wa binadamu. Chanzo cha jipu mara nyingi ni sumu ndani mfumo wa damu inayosababishwa na kutokula chakula kinachostahili.

Unapobaini una jipu usihangaike, tumia jani la tambuu kukabiliana nalo. Chuma jani la tambuu, lipake mafuta ya nyonyo, bandika kwenye jipu, baada ya saa tatu ondoa jani hilo bandika jingine.

Endelea kubadilisha jani hadi jipu litakapopasuka. Likishapasuka osha kidonda paka maji maji ya kitunguu swaumu ulichokiponda au kukisaga. Fanya hivyo kila baada ya saa nane kupita hadi kidonda kitakapo pona.

Unapoweka jani la tambuu katika jipu linaharakisha kuiva na kupasuka, urojo wa kitunguu swaumu unasaidia kuponyesha haraka kidonda hususan cha jipu.
Font Awesome Icons
KAMA UNA JIPU FANYA HIVI Reviewed by Admin on 8:30 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.