NEW ALERT

recent
MAHABA

UFUTA HUSAIDIA KUPUNGUZA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI



UFUTA HUSAIDIA KUPUNGUZA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI
Mara nyingi wakati wa hedhi mwanamke kuhisi maumivu kidogo, kukisa raha, kubana kwa misuri ya miguu na mapaja huwa ni dalili za kawaida.


Lakini wakati mwingine hali huwa inakuwa mbaya zaidi, ambapo mhusika anapata maumivu makali ya mgongo, tumbo na hata maumivu wakati wa kutoka damu.


Msongo wa kisaikologia na wasiwasi huwa vinatangulia, wakati kubana kwa misuri, maumivu makali na kuanza kutoka damu kidogo kidogo vikifuatia.


Mwanamke anapokuwa katika hali hiyo na kuwa katika hali ya uoga, huwa inaathiri misuri kufanya kazi yeke vile inavyopaswa na hivyo kusababisha kuganda kwa damu na kupelekea maumivu zaidi na maumivu yanapozidi zaidi mhusika huweza kupata kizunguzungu.


Pamoja na hayo, mtaalam wa tiba asili kutoka kutoka Aljalila herbs Dr. Seif El baalawy anasema kuwa, ufuta ni moja ya tiba nzuri inayoweza kumpunguzia maumivu makali mwanamke awapo katikahali hiyo.


Mtaalam huyo anasema kuwa, ufuta unaposagwa (glasi moja) huweza kuwa ni msaada mkubwa wa kumpunguzia mwanamke maumivu wakati wa hedhi.


Anaeleza kuwa siku tatu kabla ya kuingia hedhini unapaswa kuanza matibabu kwa kuchukuwa glasi moja ya maji moto kisha ongeza nusu kijiko cha chai cha unga huo wa ufuta na ukoroge vizuri na unywe.


Endelea na tiba hii mara mbili kwa siku hadi kipindi chote cha hedhi kinapomalizika.


Hiyo ni moja ya njia inayoweza kukusaida kupunguza maumivu wakati wa kipindi chote cha hedhi


Font Awesome Icons
UFUTA HUSAIDIA KUPUNGUZA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI Reviewed by Admin on 6:21 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.