NEW ALERT

recent
MAHABA

HAYA NDIYO MAAJABU YA MDALASINI KWA AFYA YAKO



HAYA NDIYO MAAJABU YA MDALASINI KWA AFYA YAKO
Mdalasini ni kiungo kinachochea harufu nzuri na hamu ya kula kwenye vyakula na vinywaji mbalimbali. Ni msaada pia katika masuala ya kitiba. Unasaidia kuondoa maumivu ya vidonda vya tumbo, kuchochea uzazi kwa kinamama na kuondoa maumivu ya kifua.

Pia unakuepuka na hatari ya kupata magonjwa ya moyo, unaondoa sumu mwilini, kuimarisha afya ya kinywa, afya ya ngozi na kuondoa chunusi, kutibu matatizo ya kibofu cha mkojo, hupunguza uwezekano wa kupata saratani na kuongeza utendaji kazi wa ubongo.

Kazi nyingine ya kiungo hiki ni kurekebisha kiwango cha kisukari mwilini na kukuepusha na hatari ya kupata ugonjwa huo, inatibu fangasi za sehemu za siri kwa kinamama, huondoa uvimbe na maumivu ikiwa umeng’atwa na mdudu kama ng’e na kuimarisha mifupa na kuondoa maumivu ya misuli.

Kwa vidonda vya tumbo, mdalasini umeonesha ufanisi mkubwa, unaondoa tindikali ya gastiki ambayo ndiyo chanzo cha vidonda vya tumbo.

Mdalasini ambao ni gome, saga ili kupata unga utumie kijiko cha chai katika uji usio mzito au katika asali. Hii hupunguza pia maumivu wakati wa hedhi na kifua cha kubana.

Mdalasini wenye nyuzinyuzi lishe ‘fibre’ madini ya manganizi, kalisiamu, chuma na vitamini K ni vema utumie mara mbili kutwa katika maji ya uvuguvugu, uji usio mzito au katika asali kama nilivyoeleza hapo juu.

Wakulima hustawisha mdalasini kama zao la biashara ambapo wanaweza kupata mavuno mengi na bora iwapo watazingatia kanuni na taratibu za kilimo hicho.

Visiwa vya Zanzibar ni maarufu zaidi kwa kilimo cha zao hilo. Mti wa mdalasini tangu upandwe unaweza kudumu kwa zaidi ya miaka 20. Magome hutumika kama kiungo, majani yake hutumika kutengenezea mafuta.

Kitiba mmea huu una faida nyingi kwa kuwa unatibu magonjwa mengi kama nilivyotaja hapo juu. Unaondoa ugumba kwa mwanaume na utasa kwa mwanamke.

Mwaume atumie vijiko viwili vya unga wa magome ya mdalasini achanganye na asali katika mlo wa jioni. Kwa mwanamke inaimarisha na kuhamasisha kizazi.

Kwa wale tasa watumie kipimo cha mwanaume kila siku kwa miezi kadhaa wataona mujiza ukifanyika.

Tumia vijiko viwili vya asali na vitatu vya unga wa mdalasini koroga pamoja kwenye maji moto na kunywa itaondoa asilimia 10 ya lehemu (chorestrol) mwilini mwako.


Kwa maradhi ya mafua tumia kijiko kimoja cha chai cha asali na kingine cha unga wa mdalasini mara mbili kwa siku muda wa siku mbili, mafua na kikohozi vitaondoka.

Tatizo la kunyonyoka nywele, tumia kijiko kimoja cha unga wa mdalasini na kingine cha asali na kingine kidogo cha mafuta ya mzeituni changanya pamoja, paka kichwani viache kwa muda wa robo saa kisha osha kichwa.

Endelea mara moja kwa siku, kila siku utaona mtokeo bora ya afya yako.

Mdalasini pia unazuia na kuondoa au kufukuza gesi tumboni, kutia joto tumbo lililopoa, vidonda vya tumbo, kichefuchefu, kutapika na kuharisha.

Mmea huu pia unasaidia kusukuma mbele muda wa kuingia katika hedhi baada ya kujifungua. Siku ya kujifungua tafuna kipande cha mdalasini mfululizo kwa muda wa siku 30 utachelewa kuingia hedhi kwa muda wa mwaka na nusu au miaka miwili na hivyo itazuia usipate mimba kwa wakati usiotakiwa.

HAYA NDIYO MAAJABU YA MDALASINI KWA AFYA YAKO Reviewed by Admin on 2:46 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.