NEW ALERT

recent
MAHABA

ONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI





Harufu mbaya mdomoni ni tatizo ambalo huwapata baadhi ya watu. Mara nyingi waathiriwa hawajitambui kuwa wana tatizo hilo huku marafiki zao wa karibu nao hukosa ujasiri wa kuwaeleza.

Kimsingi tatizo hilo linasababishwa na kuoza mizizi ya meno, matatizo ya fizi, kuwemo mashimo katika meno ambayo hutunza mabaki ya chakula au matatizo ya mfumo wa upumuaji wa hewa kama mapafu, pua na koo.

Matatizo katika uyeyushaji chakula na kufunga choo mara kwa mara nayo huchangia tatizo la harufu mbaya mdomoni. Zipo tiba asili za aina nyingi ambazo zinaweza kuwa msaada kwa tatizo hilo. Leo nakuja na pera pamoja na juisi ya matunda na mbogamboga.


Ukibaini una tatizohilo, kula pera bichi, ndani ya pera mna dawa ya kuua wadudu mdomoni. Kula pera kubwa moja bichi kila asubuhi baada ya kupata kifungua kinywa.


Pera husaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni na kuponyesha fizi zinazotoa damu. Ikiwa eneo ulilopo hakuna mapera basi tafuna majani matatu ya mpera kila baada ya mlo wa asubuhi.


Au kunywa juisi ya matunda na mbogamboga ni chanzo kizuri cha viini vinavyohitajika kukabiliana na tatizo hilo. Mtu mwenye harufu mbaya mdomoni anahitaji kula vyakula vyenye viini vinavyosaidia kukabiliana na tatizo hilo.


Hivyo, ni vema mgonjwa ahakikishe anakunywa juisi ya matunda au kula matunda yenye na juisi ya mbogamboga au kula mbogamboga zenyewe katika milo yote. Hakikisha mboga na matunda vimeoshwa vizuri kwa maji safi na salama, epuka kuzipika kwa muda mrefu.


ONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI Reviewed by Admin on 1:45 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.