NEW ALERT

recent
MAHABA

KABICHI INAONGEZA DAMU NA KUTIBU VIDONDA VYA TUMBO

KABICHI INAONGEZA DAMU NA KUTIBU VIDONDA VYA TUMBO
KABICHI NA FAIDA ZAKE. Kabeji ni moja... - Muu Herbal Clinic ...
Kabichi ni mboga yenye umbo la mviringo. Imo katika kundi la mboga za majani. Mboga hii ni msaada mkubwa kwa kuimarisha afya ya binadamu.


Ina nguvu ya kupambana na changamoto mbalimbali za kiafya. Kabichi ipo ile yenye rangi nyekundu, bluu na kijani ndiyo imezoeleka na wengi hapa nchini.


Miongoni mwa faida zake ni pamoja kurahisisha tendo la usanisi wa chakula tumboni na kuongeza damu mwilini hususan kwa kabichi yenye rangi ya nyekundu.


Juisi ya kabichi inasaidia matatizo mbalimbali kama kuondoa kizunguzungu na maradhi ya vidonda vya tumbo. Pia ichemshe kabichi, kisha mimina maji yake acha yapoe hadi kiwango cha uvuguvugu kisha ayakalie anayesumbuliwa na tatizo la mgolo yatasaidia kuurudisha ndani.


Kwa wajawazito ni vema wasiitumie mboga hii yenye asili ya asidi nyingi kwani wanaweza kusababisha mimba kuharibika. Kabichi pia unaweza kutengeneza saladi au kachumbari inayotumika kuongeza ladha kwenye mlo.


Ulaji wa mboga hii iliyotayarishwa kwa kuzingatia kanuni zote za kiafya ni msaada mkubwa kwa miili yetu. Vitamini K inayopatikana katika mboga hii inafanya kazi kama chakula cha ubongo, kabichi inasaidia kwa kiasi kikubwa mlaji kuwa na uwezo mzuri wa kufikiri.


Kwa mujibu wa jarida la Health Living kabichi ina uwezo wa kuzuia na kukabiliana na magojwa mbalimbali nyemelezi kwa ubongo. Vilevile inatajwa kupunguza makali ya ugonjwa wa saratani ya matiti kwa wanawake.


Inaelezwa kuwa tishu zilizopo ndani ya mboga hii zinazuia kukua kasi ya ugonjwa wa saratani ya matiti. Kwa wenye tatizo la kuumwa kichwa mara kwa mara supu inayotokana na kabichi iliyochemshwa ni dawa inayoweza kukabiliana na hali hiyo ndani ya muda mfupi.

Kwa wenye ngozi yenye mafuta na kushambuliwa na chunusi sugu kabichi ina uwezo wa kukausha mafuta na kuiacha ikiwa kwenye hali ya ukavu.


Mboga hii pia ni kichocheo katika mzunguko wa damu, ukila inasaidia kuifanya itiririke na kuzunguka vizuri katika mishipa yake.

Ikiwa una tatizo lolote la kiafya, karibu katika kituo chetu cha kutolea huduma za afya Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam. Tunajali mgonjwa wa aina yoyote, tunatumia tiba lishe na virutubisho kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya.

KABICHI INAONGEZA DAMU NA KUTIBU VIDONDA VYA TUMBO Reviewed by Admin on 2:39 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.