UJUE MNANAA NA SIRI YAKE KITIBA
UJUE MNANAA NA SIRI YAKE KITIBA
mnanaa mimiafya.com |
Zipo aina mbalimbali za mimea inayotumiwa na wataalamu wa tiba asili kuganga afya za wanaosumbuka kwa maradhi tofauti tofauti.
Ninapozungumzia mimea, wapo ninaowagusa moja kwa moja ambao wanakumbuka jinsi ilivyowaokoa baada ya kuhangaika huku na huko kwenye tiba za kisasa kwa muda mrefu bila mafanikio.
Binafsi nitazungumzia aina moja ya mmea ambao ni mujarabu kwa shida nyingi za kiafya hususan zinazosababishwa na sihr (maradhi yanayosababishwa na mkono au vijicho vya watu, mapepo na aina zote za magonjwa yasiyoonekana hospitali).
Mmea huo ni mnanaa. Baadhi ya watu wanasumbuliwa na tatizo la mwili kuuma na vitu visivyoonekana machoni kuwatembea mwilini, wengine wanapoteza fahamu au kumbukumbu mara moja au mbili kwa wiki, wengine kusahau ambako kunapelekea afya ya akili zao kuteteleka. Kwa ujumla watu wanaougua maradhi ya sihr mmea huu ni msaada mkubwa.
Unaweza kutumia unga wa majani ya mmea huu au wa mbegu zake. Mnanaa unaojulikana kama mint kwa lugha ya kigeni, una kemikali nyingi hivyo ni vema matumizi yake yazingatie maelekezo kutoka kwa mtaalamu.
Iwapo unatumia unga uliotokana na mbegu za mnanaa chukua kijiko kimoja kidogo weka katika lita moja ya maji kisha chemsha muda wa dakika 10 hadi 15, ikishapoa kunywa nusu glasi jioni kabla ya kulala.
Kunywa mara moja kwa siku tena ni jioni tu. Fanya hivyo pia kama utatumia unga uliotokana na majani makavu ya mnanaa uliokausha. Lakini ni vema kabla ya kutumia tukawasiliana kupitia namba zangu za simu hapo chini.
UJUE MNANAA NA SIRI YAKE KITIBA
Reviewed by Admin
on
2:32 PM
Rating:
No comments: