KUKOSA HEDHI KWA WANAWAKE
KUKOSA HEDHI KUNAVYOWAWEKA WANAWAKE KATIKA HATARI YA KUTOPATA WATOTO
Mara nyingi nimekuwa nikitoa elimu kuhusu magonjwa mbalimbali ya wanawake kama maambikizi katika njia ya mkojo (U.T.I), maambukizi katika via vyao vya uzazi na maumivu makali wakati wa hedhi.
Leo nimeona nizungumzie kuhusu tatizo la kukosa hedhi linalowakabiliwa baadhi ya wanawake wenye umri mdogo wa miaka 18, 26 au hata 30. Umri wa mwanamke kukoma hedhi ni kuanzia miaka 45 na kuendelea.
Miongoni mwa wanawake hao wanaokosa hedhi wapo ambao wanakaa miezi sita, wengine mwaka na wapo ambao hawajawahi kuingia hedhi kabisa tangu wazaliwe.
Zipo sababu nyingi zinazochangia tatizo hilo ambapo ni pamoja na msongo wa mawazo, kusinyaa kwa ovari ya upande mmoja, kufanya mazoezi kupita kiasi, kuwa na homoni nyingi za kiume, kuota vinyweleo isivyo kawaida au kuota ndevu.
Kuna athari nyingi kwa mwanamke asiyeingia hedhi ambazo ni pamoja na kutoshika mimba kwa sababu mayai hayapevuki, kujisikia chefuchefu daima, kuvimba miguu na kizunguzungu.
Zipo njia nyingi za kuwezesha kuliondoa tatizo hilo, lakini leo nakujulisha moja ambayo ukizingatia maelekezo inasaidia sana vinginevyo kama tatizo lako ni kubwa njoo nione utapata msaada wa uhakika zaidi.
KUNGUMANGA
Kungumanga ina uwezo mkubwa wa kupevusha mayai ya mwanamke na kuondoa maumivu ya tumbo wakati wa hedhi kwa mwenye tatizo hilo.
Baadhi ya maeneo watu wanafahamu nafaka hii kuwa inatumika katika mambo ya urembo pekee kumbe pamoja na mambo hayo ina uwezo mkubwa wa kurekebisha hedhi inayotoka bila mpangilio na kuwa katika mpangilio unaohitajika.
Saga kungumanga ili kupata unga. Chota kijiko kimoja cha chai cha unga huo weka katika maji moto au uji usio mzito kunywa asubuhi na jioni muda wa wiki mbili hadi sita.
KUKOSA HEDHI KWA WANAWAKE
Reviewed by Admin
on
6:33 AM
Rating:
No comments: