SHIDA YA SHINIKIZO LA DAMU
BINZARI ni kiungo kinachotokana na mmea unaofahamika kama manjano. Hata hivyo, licha ya kuwa wapishi wanapenda kuitumia binzari kama kiungo, bila shaka si wote nwanaofahamu iwapo ina kiwango kikubwa cha matibabu.
Manjano ni zao linalostawishwa katika baadhi ya mikoa hapa nchini, baada ya kukomaa huchimbwa tayari kwa kuandaliwa kwa ajili ya kutumiwa kama kiungo au kuuzwa ambapo wakulima hujipatia fedha zinazoongeza kipato cha familia zao. Ustawishwaji wa manjano unafanana na ule wa tangawizi ambapo viungo hivyo vyote ili kutumiwa sharti vichimbwe ardhini.
Watu wengi wangekuwa na uelewa mkubwa kuhusu umuhimu wa binzari kuwa inatibu magonjwa mbalimbali basi wapishi katika familia katika jamii zetu wasinge acha kutumia kiungo hicho. Asili ya binzari ni Asia na India ambako nchi hizo zimeanza kutumia kiungo hicho kutoka karne nyingi zilizopita baada ya kubaini faida zake. Wanaotumia binzari hawawezi kuacha kuitumia kwa kuwa ina faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuifanya ngozi kuwa na nuru nzuri.
Binzari ambayo baada ya kukomaa huchimbwa kutoka ardhini ina faida nyingi mno katika mwili wa binadamu lakini pia mkulima anapata fedha kwa kuuza bidhaa hiyo adhimu. kiungo hicho pia kinarekebisha mwenendo wa mapigo ya moyo hususan kwa wenye changamoto ya shinikizo la damu. Pia anasema inasaidia kibofu cha mkojo kufanya kazi yake vizuri, lakini pia figo yenye changamoto inayotokana na kemikali au sumu ina uwezo wa kuisafisha kabisa. "Kibofu cha mkojo na figo vinashirikiana iwapo kimoja hakifanyi kazi vizuri kina athiri kingine na hivyo kuzua changamoto katika mwili mzima.
"Nchi za India, China na Asia wengi wanakabiliwa na changamoto ya matatizo ya shinikizo la damu hivyo wanatumia bizari ili kutengeneza afya ya mapigo ya moyo. "Wanaotumia binzari kwa kiwango kikubwa ngozi yao haiwezi kushambuliwa na maradhi ya ngozi, na wakati wote ngozi yao hubaki katika mwonekano wa kuwa na nuru na inayovutia,"

Reviewed by Admin
on
9:44 AM
Rating:
No comments: