NEW ALERT

recent
MAHABA

JINSI YA KUTIBU MACHO YANAYOUMA

KITUNGUU MAJI CHEUPE KINAFAA KUTIBU MACHO YANAYOUMA




Font Awesome Icons

Ugonjwa wa macho hushambulia utando mwembamba unaofunika mboni ya jicho na chini ya kope za macho. Mara nyingi mwanzoni mwa ugonjwa macho huwa mekundu pamoja na kuwasha, baadaye huanza kutoa machozi na kama tiba itachelewa tongotongo zitatapakaa machoni.


Wakati wa kuamka asubuhi unaweza kukuta macho yameziba kwa sababu ya kugandamana kwa tongotongo. Ugonjwa huu huambukizwa haraka huku chanzo chake kikiwa ni bakteria au virusi.


Nashauri kabla hujaanza kutumia tiba asilia nenda hospitali kamwone daktari ili athibitishe ni aina gani ya ugonjwa wa macho unaokusumbua kisha tumia kitunguu cheupe.


Saga kitunguu cheupe kisha kamua maji yake, weka matone matatu katika kila jicho mara mbili kutwa kwa maana ya asubuhi na jioni muda wa siku nne.


Au kama hauna kitunguu cheupe na upo jirani na mama anayenyonyesha, weka matone matatu ya maziwa ya mama katika kila jicho kutwa mara tatu kwa maana ya asubuhi, mchana na jioni muda siku nne.


Ikiwa una tatizo lolote la kiafya, karibu kwenye kituo chetu cha kutolea huduma za afya Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam. Acha kuendelea kuteseka kwa maradhi yaliyoshindikana.


Tunamjali mgonjwa yeyote, tunatumia tiba lishe na virutubisho asili kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya zinazomsumbua binadamu.

Font Awesome Icons
JINSI YA KUTIBU MACHO YANAYOUMA Reviewed by Admin on 1:29 AM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.