BARIDI YA BISI NA TIBA YAKE
UNAMAKUNYANZI YA UZEE? TUMIA KIAZI MVIRINGO
Kiazi mviringo kikipikwa au kukaangwa ni chakula kinachopendwa na wengi katika jamii nyingi. Pia kikifinyangwa na kupatikana ugali, bandika juu ya ngozi yenye tatizo au bawasiri ni msaada kwa mwenye tatizo husika.
Kiazi hiki pia ni ëtonicà nzuri ya ngozi, unatakiwa kunawia juisi yake na machicha yake bandika juu ya ngozi inasaidia kuondoa makunyanzi ya uzee na kuilainisha.
Chakula ni sehemu nene ya mizizi ambayo ndiyo kiazi chenyewe. Ina wanga, vitamini na madini. Sehemu iliyojitokeza nje ya ardhi ya kiazi hiki hailiwi kwa kuwa ni sumu.
Juisi ya kiazi hiki ni nzuri kwa tatizo la baridi yabisi, vidonda vya tumbo na asidi ya tumboni. Pia kinasaidia kwa wenye matatizo ya jongo (gout) na kinaondoa sumu mwilini.
Hata hivyo, baadhi ya viazi hivyo vikiwa shambani kuna sehemu inakuwa juu ya ardhi ambayo hubadilika rangi kuwa kijani, hiyo isiliwe kwa sababu ina chembe chembe za sumu ijulikanayo kama ‘solanineÃ, inaathiri via vya uzazi.
Pamoja na mambo mengine kiazi hiki chenye majina mengi kama kiazi cha kizungu, kiazi Ulaya, kiazi mviringo au mbatata, ni mmea wa chakula uliomo katika familia ya Solanaceae.
Ni chakula muhimu kimataifa. Asili yake ni Amerika Kusini. Wahispania walikikuta Amerika na kukisambaza Ulaya. Wakati mwingine kinaitwa ‘kiazi Ulaya’ au ‘kiazi kizungu’ kwa sababu kimekuja Afrika kikitokea Ulaya.
BARIDI YA BISI NA TIBA YAKE
Reviewed by Admin
on
2:09 AM
Rating:
No comments: