MIMBA YA MWEZI WA NNE
Wahenga walisema kuwa ‘ngoja ngoja huumiza matumbo’. Lakini sasa kuna ‘subira ambayo huvuta heri’.
Mimba ya miezi minne huwa rahisi sana kwa wanawake wengi. Waliokuwa na dalili za ugonjwa hapo awali huanza kuonyesha heri zaidi wakati wanapofikisha mimba katika mwezi wa nne.
Tukizungumzia tu kwa ufupi, dalili za kuonyesha kuwa una mimba ya mwezi wa nne, yafwatayo ni yale ya kawaida baina ya wanawake wengi duniani.
Dalili za mimba ya mwezi wa nne
- Kuongeza Kilo (Weight gain).
- Kuhisi Kujikunakuna haswaa tumboni na kwa matiti (Itchy skin around your growing tummy and breasts).
- Alama Ya kunyoosha ngozini (Appearance of stretch marks).
- Uzito wa kupumua (Labored breathing).
- Kuhisi njaa (Hunger).
- Uchechoaji wa moyo na kutokuwa na ulaji nzuri (Heartburn and indigestion).
- Ongezefu wa nishati au nguvu (Increased energy).
- Mishipa ya Vurugu (Varicose veins).
Kuongeza kilo
Ukishafikisha mimba ya miezi minne, Utaanza kuona ya kuwa umeongeza kilo wa kiasi fulani. Kuna wale waliopunguza kilo kwa ajili ya kutapika hapo awali. Lakini Mwezi wa nne wa mimba huwa na heri njema. wanawake wengi huanza kupata nafuu zaidi.
Kuhisi Kujikunakuna haswaa tumboni na kwa matiti
Kwa sasa matiti yako yamekuwa makubwa kiasi fulani. Kwa hivyo Kufura kwa matiti yamefanya ngozi yako kupanuka. Hii ndio sababu unaweza kuhisi kujikunakuna. Pia tumbo lako limenza kukua kubwa kiasi kwa sababu mtoto wako ameanza kukuwa mkubwa. Hivi basi waweza kujikunakuna tumboni, miguuni, mikononi, na kadhalika.
“Mwenye kupata mtoto hakosi mbeleko”
Alama Ya kunyoosha ngozini
Katika Miezi minne ya mimba, alama ya kunyoosha huanza kuongezeka na kuonekana baina ya wanawake wengi walio na uja uzito. Alama hii huonekana upande wa matiti, tumboni, mikononi upande wa nyuma ya misuli, makalioni na miguuni. Alama hii huonyesha kuwa ngozi yako inajinyoosja kwa ajili ya kuongeza kilo.
Uzito wa kupumua
Hapo awali ulipokuwa bila ujauzito, Uliweza kupumua kwa urahisi hata baada ya kufanya kazi ngumu au baada ya kufanya mazoezi ungeweza kuipata pumzi baada ya muda mchache. Ukishapata mimba na unaendelea kimiezi, Utaanza kufahamu ya kuwa umekuwa mwepesi wa kupumua. Mwezi wa nne wa mimba huonyesha zaidi ya kuwa kipimo cha pumzi yako imekuwa ndogo zaidi. Unaweza kufanya kazi ndogo lakini kupumua kwako ni kama wa yule aliyeshiriki katika mbio.
“Mwana mkuwa nawe ni mwenzio kama wewe”
Kuhisi njaa
Unaweza kufikiria mbona unakula kila wakati. Mwezi wa nne wa mimba huwa na hamu kubwa ya kula vyakula vingi na vya aina mbalimbali. Jaribu kuwaza kuwa umekuwa na ugonjwa wa asubuhi na sasa umeanza tu kupata nafuu na hamu yako ya kula umerudi kwa wingi. hali hii ni nzuri kwa mwanamke yeyote aliye na mimba kwa sababu mwanawe pia anaweza kujimudu kiafya kupitia vyakula unavyovila.
Uchechoaji wa moyo na kutokuwa na ulaji nzuri
Tulivyozungumzia hapo awali, uchocheaji wa moyo hufanyika wakati homoni mbalimbali yanazidi kuongezeka mwilini. Homoni progesterone hufanya ulaji kuzozea na hii inaweza kuongeza dalili za uchocheaji moyo.
Ongezefu wa nishati au nguvu
Wakati huu, Umeanza kuhisi ya kuwa una nguvu zaidi ya kawaida tangu uliposhika mimba. Unaweza kufanya kazi ya nyumba bila msaada na pia unaweza kutembea kwa muda mrefu bila kuhisi uchovu zaidi. Hii ni kwa sababu mwanako amejilaza vyemya chupani mwako na pia ameanza kujitegemea kiasi.
Mishipa ya Vurugu (Varicose veins)
Pia, Mishipa ya vurugu hutokea kwa zaidi mwezi huu wa nne wa mimba, Damu yako imeongezeka sana na mishipa yako yanafanya kazi kubwa ya kumtengeza mwana ili awe na afya nzuri, kuongezea kuimudu mwili wako. Kwa sababu ya kazi halisi inayoendela mwilini mwako usiku na mchana, Mishipa ya vurugu huendelea kujionyesha kwa wingi, sanasana upande wa miguuni.
“ Mwana mwema ni taji tukufu kwa wazazi wake”
Haya basi hebu tuyatafakari yale tushazungumzia hapo awali, Unahisi dalili hizi zote na unafurahia ya kuwa ni za kawaida. Lakini akilini unawaza jinsi mwanawe anaendelea kukua. Hebu basi tuangalie jinsi mwanawe amekuwa tangu miezi mitatu.
Hatua za maendeleo wiki wa kumi na tatu hadi wa kumi na sita
Mwanawe amefanya hatua kubwa ya maendeleo mwilini mwake. Katika wiki wa kumi na tatu, alama za vidole vyake huanza kujionyesha, ingawaje ngozi yake bado ni laini zaidi. Mwili wake umeanza kukuwa na kuwa na usambamba ili kulinganisha kichwa chake kililichokuwa kubwa zaidi hapo awali.
Ukiwa unamtegemea msichana, tumbo wake wa uzazi umeanza kuwa na mayai takrimu milioni mbili. Kimo chake sasa ni wa inchi tatu na ametoshana na kikapu cha peas (Pea pod). Pia ana kilo wa mililita ishirini na tisa.
Wiki wa kumi na nne
Wiki hii ni ule wa mabadiliko makubwa maishani mwa mtoto wako aliye chupani. Kwa sasa, Yuaweza kulikunja uso wake, Misuli ya uso wake umeanza kufanya mazoezi kama vile kutabasamu, kushangaa na kadhalika.
Figo yake yameanza kutengeneza mkojo ambayo hutoka kupitia maji ya amniotic iliyomzunguka. Kitendo hiki kitaendelea hadi wakati atakopozaliwa.
Anaweza kulikunja ngumi kwa wakati huu pia. Na pia anaweza kunyonya kidole kwa sasa ili kujifunza kunyonya na kuongeza misuli mdomoni ili aweze kunyonya wakati anapozaliwa.
Ana kilo ya mililita arobaini na nne, na kimo cha inchi tatu na nusu. Mwili wake sasa umeanza kukuwa kwa haraka na kichwa chake kimetulia shingoni ambayo sasa imeanza kuonekana.
“Mwongoze mtoto katika njia inayofaa”
Wiki wa kumi na tano
Sasa mwanawe amefikisha kimo cha inchi nne na ana uzito wa kilo ya mililita takriban sabini na tatu. miguu yake ni ndefu sasa zaidi ya mikono, na anaweza kusongesha miguu na mikono yake. ingawaje macho yake yameziba, anaweza kujua wakati kuna pambazuko au taa. Ni kama vile tu Unaweza kujua kuna nuru kama umeziba macho yako.
Wiki kumi na sita
Ni wakati mwana wako ameanza kukua mara mbili zaidi. Wiki zinazofuata ataongeza kilo maradufu na urefu pia. Kwa sasa, ana uzito wa kilo ya mililita mia moja na tatu na kimo cha inch inne na nusu. Ameanza kumea makucha vidoleni mwa miguu. Moyo wake umeanza kusambaza damu kwatsi ishirini na tano kila siku.
Kwa ukubwa ametoshana na tunda la avocado.
“Aliye na mwana na akanye”
Mabadiliko mwilini mwako
Ukishafika kuwa na mimba ya miezi minne, utagundua mabadiliko haya wa nje kama vile:-
- Matiti yako yamekuwa makubwa
- Umeongeza kilo
- Umerudi kuwa na nguvu na unahisi nafuu
- Uchungu wa matiti umeanza kudidimia
- Tumbo lako limeanza kuonyesha kuwa una mimba
- Unaweza hisi kana kwamba una homa. Hii ni kawaida
- Unaweza kuhisi mtoto akisonga ndani ya tumbo. Wanawake waliopata mimba hapo awali wanaweza kuhisi mwana akisonga au akipiga mateke madogo wanapofikisha wiki kumi na sita ya mimba.
Mabadiliko yanayofanyika ndani ya mwili wako haswa mwezi wa nne ni, matiti yako yameanza kuunda maziwa ambayo mwana atanyonya punde tu atakapozaliwa. Maziwa haya huitwa Cholestrum na huwa na kila aina ya vyuma vya kumwezesha mtoto akue kwa njia bora atakapozaliwa.
Swala Nyeti
Je ni vizuri kulalia upande wa tumbo wakati nina mimba?
Jibu:-
Wakati una mimba, mwezi wa kwanza hadi wa tano unaweza kulala upande wowote ambayo itakufanya upate mapumziko shwari.
Lakini ukishafikisha mwezi wa tano na kuendelea, madakitari Nchini mbalimbali husema kuwa kulala upande wa kushoto ni muhimu kwa sababu hewa safi itapitishwa kwa mtoto. Wao hukana ya kuwa wakati mtoto ameanza kuwa mkubwa chupani mwa mamake, ni vizuri sana kuzingatia hali ya mapumziko haswaa ya kulala.
Usilalie mgongoni mwako kwa sabababu mwana ataufinya mshipa ambayo husindikiza damu miguuni mwako. Hii ndio sababu wanawake wengi hushikwa na kizunguzungu au hufura miguu zaidi wanapoamka.
Upenyo wa haraka
Mimba ya miezi miine ni ya kusherehekewa kwa sababu mwanamke ameanza kupata nafuu kutokana na dalili za upataji mimba. Kwa hivyo ni vizuri kuzingatia mashauri kama ifwatayo:-
- Kupata mapumziko mema
- Kula vyakula halisi na bora
- Kufanya mazoezi kila siku
- Kupumua kwa undani kila wakati
- Kujipaka mafuta tumboni na miguuni au kila mahali ili ngozi yako isiwe na alama nyingi ya kujinyoosha
- Kunywa maji mengi
- Kula kila wakati unapohisi njaa
- Unapokuwa na ufupi wa pumzi wakati ufanyapo kazi, Pumzika.
- Nena na dakitari wako unahisi tashwishwi yoyote;.
MIMBA YA MWEZI WA NNE
Reviewed by Admin
on
12:34 AM
Rating:
No comments: