NEW ALERT

recent
MAHABA

MIMBA YA MWEZI WA TANO



” Mzazi hakati tamaa”
Mwezi wa tano ya mimba huwa alama ya kuwa umefikisha nusu ya ujauzito kwa wanawake wengi ulimwenguni.
Ukijitazama kwa wakati huu, umeanza kuonyesha mimba zaidi. kuna wanawake wengi walioanza kufanya  ununuzi wa nguo mpya kwa ajili nguo zao zimeanza kuwa ndogo. Ni vizuri kununua nguo ambazo zina uhuru wa kutembea na kuinama au unapolala.
Ni wakati mwingine ambapo maswali umekujaza mawazoni na ungependa kujua mengi juu ya mimba ya miezi mitano. Kwanza, Ni muhimu kujua ya kuwa umefanya vema zaidi kufikisha mimba hadi mwezi huu. Wakati unayoyoma na mwanawe atakuwa mikonoi mwako hivi karibuni.
Kila mwezi ya kuwa na mimba huwa na dalili zake. Kwa ufupi, Hebu tutazame dalili hizi katika mwezi wa tano.

Dalili za mimba ya mwezi wa tano

  • Vipepeo tumboni (butterflies in your Stomach)
  • Uchocheaji wa moyo (Heartburn)
  • Uvimbiko (Constipation)
  • Kuhisi kizunguzungu (Dizziness)
  • Ufupi wa  pumzi(Shortness of breath)
  • Kutokwa na damu puani (Nose bleeding)
  • Kutokwa na damu kwenye fizi (Gum bleeding)
  • Kukosa usingizi na starehe ya kulala (uncomfortable sleeping positions and insomnia)
  • Kujikunakuna (Itchiness)
  • Kufura mikono na miguu ( Swollen hands and feet)
Hebu tuyafafanue dalili hizi. Lakini kwanza hebu tafakari methali hii:-
Pendo la mwana liwa magoni kwa nina”

Vipepeo tumboni

Mwezi wa tano wa  ujauzito huja na furaha kiasi kwa sababu, mwanawe anaposonga au kupiga mateke, Unaweza kuhisi ni kana kwamba una vipepeo tumboni. Hii ni chanzo kubwa kwa mama kuanza kujadiliana na mwanawe.

Uchocheaji wa moyo

Hali ya kiungulia moyo huendelea katika mimba ya Miezi Mitano, na wakati mwingi uchungu kifuani huongezeka  zaidi wakati unapotembea au unapofanya kazi ngumu.

Uvimbiko

Wakati una ugumu wa kuenda haja na pia unahisi ni kana kwamba umefura tumbo, Ni muhimu sana kunywa maji mengi haswaa mwezi wa tano ya mimba na miezi zijazo. kwa sababu, Uvimbiko huendelea hata baada ya kujifungua.

Kuhisi kizunguzungu

Mwana anapoendelea kuwa mkubwa, kuna mishipa mwilini ambayo huongoza damu kila upande. Mishipa hii ikifinyika, hufanya mzunguko wa damu kuenea mwilini pole pole sanasana wakati mwanamke anapolalia upande wa mgongo, au anapofanya kazi nyingi ambayo husababisha uchovu kwa urahisi. Unapofikia mimba mwezi wa tano ni muhimu kuchukulia shughuli zote kwa urahisi.
“Mwenda pole hajikwai”

Ufupi wa  pumzi

Unaweza kuhisi ya kuwa una ufupi wa pumzi wakati unapotembea au kufanya kazi mabalimbali. ni wakati wako wa kuchukua muda wa kupumua na kufanya mapumziko wakati unahisi uchovu. Dalili hii ni ya kawaida mno na hujulisha wanawake wengi wakati wao wa mapumziko umewadia na wanastahili kutilia maanani.

Kutokwa na damu puani

Mimba inaweza kufanya mishipa ya damu puani mwako kufura na pia kwa sababu ukiwa na mimba kuongezeka wingi wa damu mwilini huwa kawaida, hivyo basi shinikizo la damu huwa juu na mwanamke mja mzito anaweza kutokwa na damu puani kwa urahisi. madakitari wengi husema hii ni kawaida na sio hatari.

Kutokwa na damu kwenye fizi

Karibu wanawake asilimia nusu ambao ni waja wazito, huwa na fizi ambazo zimefura, au nyepesi. Wakati mwanamke mja mzito anaposugua meno, yuaweza kugundua kuwa kuna damu kwenye mate au kisugua meno. Hii ni dalili ya fizi kuwa na masumbuko kiasi. Wakati homoni yako hubadilika, inaweza kuufanya fizi kuwa nyeti.

Kukosa usingizi na starehe ya kulala

Usingizi ni muhimu sana kwa kila binadamu. Lakini unapokuwa na mimba haswaa wakati wa miezi ya tano na kuendelea, wanawake wengi huanza kupoteza usingizi wao. Wanawake wengi huwa na usingizi mwingi wakati wa miezi ya kwanza wa kushika mimba. Kwa hivyo wanapoanza kukosa usingizi, wao huwa na maswali mengi na mawazo juu ya ni kwa nini hawawezi kulala. Mimba huweza kukufanya uchoke siku nzima hadi unapotaka kulala usiku, huwezi. Pia, wakati unapoanza kuwa na tumbo kubwa, Kulala huwa ngumu kwa sababu upande wa kulala hubadilika muda kwa muda.
“Pikia mzazi nawe upate tonge”

Kujikunakuna

Wakati damu huongezeka mwilini, na pia mwili wako unapoanza kunenepa kwa ajili ya ujauzito, unaweza kuhisi kujikunakuna sehemu mbalimbali mwilini. Kuna wale ambao huanza kujikunakuna kichwani, tumboni , miguuni, mikononi, na pia sehemu nyeti. Ni vyema kuzingatia vyakula unavyovila na pia kujipaka mafuta mwilini na kuhakikisha ya kuwa unakunywa maji mengi.

Kufura mikono na miguu

Kufura ni kawaida wakati wa ujauzito. Hii ni kwa sababu ya uongezeko wa damu mwilini. Kufura ya kawaida ambayo huitwa ‘edema’, huonekana mikononi, usoni, miguuni,  na kwenye fundo la miguu. Hali hii ya kuhifadhi maji mwilini ni muhimu ili mwili wako uwe mwepesi na kupanuka wakati mtoto anapokua chupani mwako.
“Asiyesikia la mkuu, huvunjika guu”

Hatua za maendeleo wiki wa kumi na saba hadi wiki ishirini

Katika wiki wa kumi na saba mwana wako ameanza kuwa na mifupa nyepesi. Ukamba wake wa utovu ambao humlisha wakati yumo chupani, umeanza kuwa imara na nene. kwa sasa ana kimo cha Inchi tano na kilo ya mililita mia moja arobaini na nane, karibu na kilo ule wa mboga ya tanipu. Yuaweza  kuusongesha viungo vyake na tezi zake za jasho pia zimeanza kuumbika.
“Radhi ya mama tamu”

Wiki wa Kumi na nane

Kutoka Kichwani hadi kitako chake, mwanawe ana kimo cha inchi tano na nusu. ana kilo ya mililita mia mbili na saba.
Anashughulika kuukunja vidole vyake vya mikono na miguu, pia kuukaza misuli yake mwilini. Mishipa yake ya damu yameanza kuonekana ngozini mwake. Na masikio yake yako kwenye pahali pa usahihi. kama una msichana neli yake ya uzazi (Fallopian tube) ushaumbika. Kama ni mvulana sehemu zake za siri pia ushaumbika wakati huu.

Wiki wa kumi na tisa

Mwanako amefikisha kimo cha inchi sita, na ana kilo cha mililita mia mbili hamsini na moja. Kuna ugunduzi ya kuwa mwanawe anaweza kusikia sauti lako wakati huu. Unaweza kumzungumzia au kumsomea kitabu. ana uzito wa nyanya kubwa.
Yuandelea kutoa mkojo na nywele kichwani chake pia kimeanza kuonekana. Mwili wake umezungukwa na nta ambayo hulinda ngozi yake.
“Shime ya ngoma ina mzazi”

Wiki wa Ishirini

Mtoto wako amefikisha urefu ule wa ndizi. Ana kimo cha mililita mia tatu na kumi na urefu wa inchi sita na nusu. Yuaweza kumeza. Hii ni vizuri kuutengeneza mfumo wake wa mmeng’enyo wa chakula.

Mabadiliko mwilini mwako

  • Kituo cha uzito chako kimeanza kubadilika kwa sababu ya kukuwa na tumbo kubwa. kwa hivyo unaweza kuwa mwepesi kwa matembezi yako na ni muhimu kujivisha viatu vya chini.
  • Macho yako yanaweza kukauka. ni vizuri kunywa mazi mengi.
  • Uongezaji wa hamu ya vyakula.
  • Mfumo wa mzunguko wa damu yako inapitia mabadiliko nyingi. Unaweza kuhisi Kizunguzungu unaposimama kwa haraka.
  • Tumbo lako limeanza kuonekana kubwa zaidi ya miezi iliyopita. na umeanza kuongeza kilo kwa haraka.
  • Uchungu tumboni mwa uzazi ni kawaida kwa sababu ya kiuono chako kupanuka.
  • Ngozi yako pia inaanza kubadilika. Kiganja cha mkono wako huweza kuwa nyekundu.
  • Vipacho vya Ngozi nyeusi mwilini mwako.
  • Pia kwa ajili umefikisha hatua nusu ya kuubeba mimba, Unaweza kuhisi ya kuwa una nguvu zaidi.
  • Kuwa na joto jingi haswaa wakati wa usiku unapolala.
  • Kutoka kitandani huwa ngumu zaidi.
“Tumbo ni shamba”

Swala Nyeti

Je ninaweza kufanya mazoezi yapi nikiwa na mimba?
Mwanamke mja mzito anaweza kuufanya mazoezi mbalimbali wakati ana mimba . Mazoezi haya hutegemea na mwili wa kila mwanamke. Ni vizuri kuzingitia mazoezi miepesi kama vile kutembea na kupumua hewa safi  kwa undani kupitia pua lako na kuutoa kwa mdomo kila mara.
Unaweza pia kujinyosha muda kwa muda.
Kuna wanawake wengi ambao huendelea na shughli zo kama kawaida kama vile wakulima. Ni muhimu kujua ya kuwa maisha ya mwengine inakutegemea ili kupata afya njema. Ni vizuri kushauriana na dakitari wako ili ujue jinsi ya kujitunza wakati umebeba ujauzito.

Upenyo wa haraka

  • Zingatia viatu vya usalama ili usiweze kuanguka na kuhatarisha maisha yako na ule wa mwanawe.
  • Unywaji wa maji mengi.
  • Unapolala ni vizuri kuulalia upande wako wala si mgongoni au tumboni.
  • Ni wakati mzuri wa kushauriana na dakitari wako ili akueleze mengi juu ya ukuzi wa mimba yako. kama ni ya salama au unatakikana kuzingatia maswala fulani.
  • Kwa sababu una hamu ya vyakula vingi zaidi, Ni viuri kutilia maanani ulaji wa vyakula bora.
  • Kula vyakula vyenye vyuma ili kuongeza damu yako.
  • Ukiwa na machungu miguuni, jaribu kuinua miguu, kupata usuguaji kutoka kwa mpenziwe au kuuweka ndani ya beseni ya maji joto.
Kwa haya na mengi, ungana nasi tutakapozungumzia mimba ya Mwezi Wa Sita katika sura ifwatayo.

MIMBA YA MWEZI WA TANO Reviewed by Admin on 1:22 AM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by . © 2020
credit JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.